Pata taarifa kuu
ZAMBIA-SIASA-USALAMA-UCHAGUZI

Zambia: Guy Scott atangazwa kuwa rais wa mpito

Makamu wa rais wa Zambia Guy Scott ametajwa kuwa rais wa muda wa nchi hiyo kufuatia kifo cha rais Michael Sata aliyefariki wakati akiendelea kupata matibabu nchini Uingereza.

Rais wa Zambia aliye fariki, Michael Sata.
Rais wa Zambia aliye fariki, Michael Sata. REUTERS/Siphiwe Sibeko/Files
Matangazo ya kibiashara

Guy Scott, ambaye wazazi wake ni raia wa Scotland, anakuwa rais wa kwanza mzungu baada ya Frederick de Klerk wa Afrika Kusini wakati wa utawala wa makaburu.

Akitangaza uamuzi huo waziri wa ulinzi na sheria Edgar Lungu, amesema kuwa Scott atakaimu madaraka hayo mpaka pale uchaguzi mkuu mwingine utakapofanyika, uchaguzi ambao unatarajiwa kufanyika ndani ya siku 90.

Katika kipindi ambacho rais Sata amekuwa haonekani hadharani tayari kuliripotiwa kuwepo kwa mivutano ndani ya serikali na chama chake kila mmoja akiwania kurithi nafasi yake.

Wakti huo huo rais wa Marekani Barack Obama amejiunga na baadhi ya viongozi wengine wa mataifa ya kiafrika na dunia, kutuma salaam za rambi rambi kwa wakuu wa nchi ya Zambia kufwatia kifo cha Michael Chilufya Sata.

Obama ameahidi kushirikiana na serikali ya mpito ambayo itaongozwa na makamu wa rais wa nchi hiyo, ambaye ni mzungu Guy Scott, huku akiwaonya wanasiasa wa nchi hiyo kuzingatia amani ya kisiasa katika taifa hilo la Afrika.

Guy Scott, licha ya kuwa alizaliwa Zambia, hawezi kugombea kwenye kiti cha urais kutokana na sheria ambazo hazimruhusu kugombea na fasi hiyo.

Michael Sata, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 77 katika hospitali ya London. Kifo chake kimetokea siku chache baada ya Zambia kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo.

Mwanasiasa huyo mkongwe aliingia madarakani mwezi Septemba 2011 baada ya kuongoza chama chake cha Patriotic Front, na kumshinda Rupiah Banda, ambaye alikuwa rais wakati huo na chama chake cha Movement for Multi-Party Democracy, kikiwa madarakani kwa miaka ishirini.

Rupiah Banda rais wa nne wa Zambie, Lusaka Novemba 2008.
Rupiah Banda rais wa nne wa Zambie, Lusaka Novemba 2008. (Photo : AFP)

 

Michael Sata ni rais wa pili kufariki akiwa madarakani nchini Zambia, baada ya Levy Mwanawasa.

Aliye kuwa rais wa zambia hayati Levy Patrick Mwanawasa,Desemba mwaka 2007.
Aliye kuwa rais wa zambia hayati Levy Patrick Mwanawasa,Desemba mwaka 2007. (Photo: AFP)

Levy Patrick Mwanawasa, alizaliwa Septemba 3 mwaka 1948 katika mji wa Mufulira (Rhodesia ya Kaskazini) na alifariki Agosti 19 mwaka 2008 katika mji wa Clamart 1. Levy Patrick Mwanawasa, alikua mwanasiasa nchini Zambia na Rais wa Jamhuri ya kuanzia mwaka 2002 hadi 2008. Alifariki Agosti 19 mwaka 2008 katika hospitali Percy Clamart, ambapo alikuwa hospitalini baada ya kupatwa na kiharusi katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika katika mji wa Sharm el-Sheikh nchini Misri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.