Pata taarifa kuu
UN-BURKINA FASO-MAREKANI-UFARANSA-USALAMA-KATIBA

Jumuiya ya kimataifa yatiwa hofu na hali inayojiri Burkina Faso

Ufaransa umezitaka pande husika katika machafuko yanayoendelea nchini Burkina Faso kurejesha hali ya utulivu. Wakati huo huo Marekani imesema inatiwa hofu na hali inayoendelea nchini humo, huku Umoja wa Mataifa ukimtuma mjumbe wake nchini Burkina Faso.

Machafuko yatokea Ougadougou, Oktoba 30 mwaka 2014.
Machafuko yatokea Ougadougou, Oktoba 30 mwaka 2014. REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Paris na Washington, ambao ni washirika wa karibu wa Burkina Faso, hawakuonyesha msimamo wao kuhusu jitihada za serikali ya Burkina faso za kuifanyia marekebisho Katiba ya nchi hiyo.

Ufaransa ina raia wake 3,500 waishio nchini Burkina Faso. Wizara ya mabo ya nje ya Ufaransa imefahamisha kwamba inafuatilia hali inavyoendelea nchini Burkina Faso. Msemaji wa wizara hiyo “Quai d'Orsay" ameelezea masikitiko yake juu ya machafuko yaliyotokea pembezuni mwa jengo la Bunge, huku akizitolea pande husika kusitisha machafuko hayo yanayoendelea.

Ufaransa ilikosoa vikali hivi karibuni mchakato ulianzishwa na utawala wa Blaise Compaoré wa kujaribu kuifanyia marekebisho Katiba ya nchi. Oktoba 7 mwaka 2014 rais François Hollande alimtumia barua mwenzake wa Burkina Faso, Blaise Compaoré, akimsihisi kutothubutu kuifanyia marekebisho Katiba ya nchi bila kujadiliana na makundi yote yanayohusika katika ujenzi wa Burkina Faso. Kwa sasa Burkina Faso ni mfano wa mataifa mengine ambayo yamekua yakijaribu kuizifanyia marekebisho katiba zao.

Kwa upande wake Marekani imezitaka pande husika kuheshimu taasisi ziliyochaguliwa, huku akitoleya wito jeshi na pande zingine husika kukomesha machafuko haraka iwezekanavyo.

Wakati huo huo mjumbe wa Umoja wa Mataifa, Mohamed Ibn Chambas anasuburiwa Burkina Faso Ijumaa Oktoba 31 katika jitihada za kurejesha amani nchini humo kwa ushirikiano na Umoja wa Afrika na Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika ya Magharibi (Cédéao).

Alhamisi mchana Oktoba 30, majengo ya kituo cha televisheni ya serikali yameshambuliwa na waandamanaji, hadi kusababisha matangazo ya kituo hicho kusimama kwa muda.

Jengo la Bunge limechomwa moto, huku mtu moja akiripotiwa kuawa katika maandamano hayo, ambapo waandamanaji wamekua wakikabiliana na vikosi vya usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.