Pata taarifa kuu
Nigeria-Usalama

Boko haram wateka Chibok,ambako walitekwa wasichana wa shule zaidi ya mia mbili

Kundi la wapiganaji wa Boko Haram la nchini Nigeria limedhibiti mji wa Chibok kaskazini mashariki mwa Nigeria ambako miezi sita iliyopita kundi hilo liliwateka wasichana wa shule zaidi ya mia mbili.

Wapiganaji wa Kundi la Boko Haram nchini Nigeria
Wapiganaji wa Kundi la Boko Haram nchini Nigeria AFP PHOTO / BOKO HARAM
Matangazo ya kibiashara

Kutekwa kwa wasichana hao April 14 mwaka huu kulivuta umakini wa ulimwengu kulifuatilia kundi hilo la kiislamu ambalo limekuwa likifanya vitendo vya ukatili kwa miaka mitano sasa.

Tayari Baadhi ya maofisa wa Umoja wa mataifa UN wametaka jumuiya ya kimataifa kuisaidia nchi ya Nigeria kupambana na wapiganaji wa kundi la Boko Haram ambao wameendelea kuzorotesha hali ya usalama kaskazini mwa nchi hiyo.

Kauli ya maofisa hawa iliungwa mkono na mwakilishi wa Umoja wa mataifa UN kwa nchi za ukanda wa Afrika ya Kati, Abdoulaye Bathily ambaye amesema mauaji yanayotekelezwa na kundi hili yamevuka mipaka na kutishia usalama wa nchi jirani.

Bathily amesema kuwa kwasasa anajaribu kufanya kila linalowezekana kuhakikisha wito wake unapata uungwaji mkono toka jumuiya ya kimataifa ili kuisaidia nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.