Pata taarifa kuu
DRC-MAMADOU-FARDC-ADF-SHERIA-SIASA

RDC: mwanga haujatolewa kuhusu kifo cha Mamadou Ndala

Uamuzi katika kesi ya watuhumiwa wa mauaji ya Kanali Mamadou Ndala unasubiriwa na wengi na huenda uamzi huo ukatolewa leo Jumatatu, Novemba 17.

Wanajeshi wa FARDC wakisindikiza jeneza la Kanali Mamadou Ndala kwa ajili ya mazishi, Kinshasa, Januari 6 mwaka 2014.
Wanajeshi wa FARDC wakisindikiza jeneza la Kanali Mamadou Ndala kwa ajili ya mazishi, Kinshasa, Januari 6 mwaka 2014. AFP PHOTO/KOKOLO
Matangazo ya kibiashara

Kanali Mamadou Ndala aliyeuawa Januari 2 mwaka 2014, baada ya gari aliyokuwemo kupigwa roketi na kuteketea kwa moto anachukuliwa kama mmoja wa mashujaa wa vita dhidi ya waasi wa M23. Raia wa Congo walifuatilia kwa karibu jinsi kesi hiyo ilivyokua ikiendeshwa, lakini wamekua na wasiwasi na mahakama juu ya kuweka wazi ukweli kwa kile kilichotokea.

Watuhumiwa zaidi ishirini walifunguliwa mashta, ikiwa ni pamoja na raia wanane, maafisa wanne waandamizi wa jeshi la Congo na walinzi wawili wa zamani wa Kanali Mamadou Ndala.

Kesi hiyo ambayo ilidumu zaidi ya mwezi mmoja, ina washtakiwa 23. Kwa muda wa wiki sita Ofisi ya mashtaka ilikabiliwa na wakati mgumu ili iweze kutoa vithibitiho na ushahidi wa kutosha, kwa kuonesha iwapo watuhumiwa hao walishiriki moja kwa moja katika mauaji ya Mamadou Ndala Moustafa.

Katika hatua ya mwisho ya kesi hiyo, mtuhumiwa mmoja tu ndiye alituhumiwa moja kwa moja kuandaa shambulio hilo Januari 2 mwaka 2014. Kanali Birocho Nzanzu alinyooshewa kidole na mmoja wa walinzi wake pamoja na shahidi mmoja aliye kuwa mpiganaji wa waasi wa zamani wa M23 kwamba alikua kati ya jeshi la Congo na waasi wa Uganda ADF-Nalu kwa kuandaa shambulizi dhidi Mamadou Ndala Moustafa.

Upande wa utetezi, ulielezea wasiwasi wake juu ya ushahidi huo. Kwa mujibu wa upande wa utetezi, vithibitishi hivyo au ushahidi huo hautoshi kwa kuweza kumtuhumu kanali Birocho Nzanzu kwamba alihusika moja kwa moja katika mauaji ya Mamadou Ndala.

Hata hivyo mtu ambaye anashukiwa kwamba angelitoa ushahidi tosha ni dereva wa Mamadou Ndala Moustafa, ambaye pia alifariki. Raia waliyokua wakifuatilia kesi hiyo tangu ilipoanza wamesema hawana imani na majaji kwamba wataweka wazi kile kilichotokea, kwani kuna uwezekano kuwa hata jeshi la Congo FARDC lilihusika katika mauaji hayo ya mamadou Ndala Moustafa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.