Pata taarifa kuu
DRC-MAMADOU-FARDC-ADF-SHERIA-SIASA

DRC: kanali Birocho ahukumiwa adhabu ya kifo

Mahakama ya Kijeshi mjini Beni Mashariki mwa Jamahuri ya Kidemokrasia ya Congo imemhukumu Kanali Birocho Kossi adhabu ya kifo baada ya kubainika kuhusika na mauaji ya Kanali Mamadou Ndala mapema mwaka huu.

Mkuu wa Mahakama ya kijeshi ya Kivu Kaskazini, kanali Joseph Maya Makako (katikati), Oktoba 1, wakati wa kuanza kwa kesi ya Mamadou Ndala Moustafa.
Mkuu wa Mahakama ya kijeshi ya Kivu Kaskazini, kanali Joseph Maya Makako (katikati), Oktoba 1, wakati wa kuanza kwa kesi ya Mamadou Ndala Moustafa. AFP PHOTO / ALBERT KAMBALE
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi katika kesi ya watuhumiwa wa mauaji ya Kanali Mamadou Ndala umetolewa jana Jumatatu, Novemba 17.

Kanali Mamadou Ndala aliyeuawa Januari 2 mwaka 2014, baada ya gari aliyokuwemo kupigwa roketi na kuteketea kwa moto, anachukuliwa kama mmoja wa mashujaa wa vita dhidi ya waasi wa M23.

Watuhumiwa zaidi ya ishirini walifunguliwa mashta, ikiwa ni pamoja na raia wanane, maafisa wanne waandamizi wa jeshi la Congo na walinzi wawili wa zamani wa Kanali Mamadou Ndala.

Mahakama hiyo pia imewahukumu watu wengine 20 na tayari wamepelekwa Kinshasa.

Kesi hiyo ambayo ilidumu zaidi ya mwezi mmoja, ina washtakiwa 23. Kwa muda wa wiki sita Ofisi ya mashtaka ilikabiliwa na wakati mgumu ili iweze kutoa vithibitiho na ushahidi wa kutosha, kwa kuonesha iwapo watuhumiwa hao walishiriki moja kwa moja katika mauaji ya Mamadou Ndala Moustafa.

Katika hatua ya mwisho ya kesi hiyo, mtuhumiwa mmoja tu ndiye alituhumiwa moja kwa moja kuandaa shambulio hilo Januari 2 mwaka 2014. Kanali Birocho Nzanzu alinyooshewa kidole na mmoja wa walinzi wake pamoja na shahidi mmoja aliye kuwa mpiganaji wa waasi wa zamani wa M23 kwamba alikua kati ya jeshi la Congo na waasi wa Uganda ADF-Nalu kwa kuandaa shambulizi dhidi Mamadou Ndala Moustafa.

Wakati hayo yakijiri vituo vitano vya redio katika miji ya Beni na Butembo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vimefungwa, kwa amri ya serikali ikivituhumu kuchangia kufanya uchochezi.

Kwa upande wake shirika la kutetea haki za waandishi wa habari nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo la “Journalistes en Danger” - JED limeelezea wasiwasi wake kuhusu hatua ya serikali ya nchi hiyo kuvifungia vituo vitano vya redio Mashariki mwa DRC ikiwa ni pamoja na vituo vya mji wa Beni na Butembo.

Aidha, shirika hilo limeiitaka serikali kuruhusu uchunguzi huru ufanyike kubaini tuhuma kuwa vituo hivyo vimechangia kufanya uchochezi, wakati vingine vilivyotajwa ni sasa zaidi ya mwaka mmoja havifanyi kazi na kusisitiza kuwa hatua iliyochukuliwa imefanyika kwa malengo maalum.

Wito kama huo pia umetolewa na raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaoishi nchini Canada, wametaka uchunguzi huru kufanyika kuhusu kufungwa kwa vituo vitano vya redio mjini Beni na Butembo, kwa madai kuwa vinashirikiana na makundi ya waasi yanayosababisha ukosefu wa usalama katika eneo hilo.

Hayo yakijiri ripoti mpya ya shirika la kimataifa la kutetea haki za bina damu human Right Watch imeituhumu polisi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwaua watu 51 wengi wao wakiwa ni vijana na wengine 33 wamlitoweka wakati wa operesheni kababmbe iliyoendeshwa na polisi dhidi ya uhuni katika mmji wa kinshasa tangu mwezi Novemba mwaka 2013 hadi Februari mwaka 2014.

Askari polisi wakijificha nyuso  wakati wa operesheni "Likofi" iliyopelekeza kutoweka kwa watu 33 na kuuawa kwa wengine 51 mjini Kinshasa  tangu mwezi Novemba mwaka 2013 hadi Februari 2014.
Askari polisi wakijificha nyuso wakati wa operesheni "Likofi" iliyopelekeza kutoweka kwa watu 33 na kuuawa kwa wengine 51 mjini Kinshasa tangu mwezi Novemba mwaka 2013 hadi Februari 2014. RFI/Habibou Bangré

Operesheni hiyo iliyojulikana kwa jina la “Operation Likofi, HRW imenyooshea kidole polisi ya Congo kwamba ilihusika na mauaji ya kikatili Shrikika hilo limeomba afutwe kazi mkuu wa polisi aliyeongoza operesheni hiyo kabla ya uchunguzi kuanzishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.