Pata taarifa kuu

Kesi ya Habyarimana: shahidi mpya raia wa Rwanda atoweka

Shahidi mpya katika kesi ya mashambulizi dhidi ya ndege ya rais wa zamani wa Rwanda Juvenal Habyarimana mwaka 1994 ametoweka tangu Alhamisi Novemba 13 baada ya kutekwa nyara mjini Nairobi nchini Kenya.

Eneo ambako ndege ya aliye kuwa rais wa rwanda Juvenal Habyarimana ilipodondokea baada ya kudunguliwa ikiwa angani kwenye uwanja wa Kanombe, mjini Kigali,usiku wa  Aprili 6 mwaka 1994.
Eneo ambako ndege ya aliye kuwa rais wa rwanda Juvenal Habyarimana ilipodondokea baada ya kudunguliwa ikiwa angani kwenye uwanja wa Kanombe, mjini Kigali,usiku wa Aprili 6 mwaka 1994. Getty/Scott Peterson
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa zilizokusanywa na RFI, Emile Gafirita alitekwa nyara mjini humo nje ya nyumba yake mtaa wa Dagoretti muda mfupi kabla ya saa sita usiku baada ya kusimamishwa na watu wawili ambao walimfunga pingu na kumlazimisha kuingia katika gari lao na baadaye kuelekea kusikojulikana.

Polisi nchini Kenya imekanusha kumtia mtu huyo nguvuni ambaye alijulikana kwa majina bandia ya Emmanuel Mugisha na kusema kuwa inachunguza suala hilo ambapo raia huyo wa Rwanda anadaiwa kutekwa na watu ambao kulingana na shahidi wa tukio hilo walikuwa wakizungumza lugha isiyoeleweka, aliiambia RFI.

Kwa mujibu wa mwanasheria wake raia wa Ufaransa, Wakili François Cantier, Emile Gafirita alikuwa tayari amekabidhiwa mwaliko ili kutoa ushahidi kuhusu tukio la kudunguliwa ndege ya aliyekuwa rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana na kumuonya kuhusu usalama wake.

Hadhi ya “Shahidi” ya Emile Gafitira katika kesi hiyo pamoja na majina yake vimekuwa vinajulikana kwa wiki kadhaa zilizopita na pande zote, ikiwa ni pamoja na viongozi wa serikali ya Rwanda ambao baadhi yao wanatuhumiwa katika kesi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.