Pata taarifa kuu
RWANDA-Kenya-Habyarimana-Mauaji ya halaiki

Rwanda: kutoweka kwa Emile Gafirita kumeibua hisia tofauti

Mpaka sasa hakuna taarifa kuhusu shahidi mpya wa majaji Marc Trévidic na Nathalie Poux aliyetoweka hivi karibuni. Emile Gafirita angelisikilizwa katika kesi ya shambulio dhidi ya ndege ya rais wa zamani wa Rwanda, Juvenal Habyarimana.

Shambulio dhidi ya ndege ya rais Juvénal Habyarimana (picha hii ni ya mwaka 1982), mwanzo wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, Aprili 6 mwaka 1994.
Shambulio dhidi ya ndege ya rais Juvénal Habyarimana (picha hii ni ya mwaka 1982), mwanzo wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, Aprili 6 mwaka 1994. AFP
Matangazo ya kibiashara

Emile Gafirita ni mwanajeshi wa zamani wa jeshi la Rwanda RDF. Alitoweka tangu Novemba 13, jioni, mjini Nairobi nchini Kenya. Kwa mujibu wa majirani zake , Emile Gafirita, alitekwa na watu wawili, ambao walimuingiza katika gari waliyokua nayo baada ya kumfunga pingu mikononi.

Emile Gafirita, alijitokeza dakika ya mwisho kuwa shahidi katika kesi ya shambulio dhidi ya ndege ya rais wa zamani wa Rwanda Juvenal Habyarimana. Mwanajeshi huyo wa zamani wa jeshi la Rwanda RDF, alijielekea hivi karibuni mbele ya vyombo vya sheria vya Ufaransa, ili aweze kusikilizwa kuhusu aliyoshuhudia wakati wa udunguaji wa ndege ya hayati rais Juvenal Habyarimana.

Emile Gafirita alijiunga na kundi la waasi wa zamani wa Rwanda (RPF), ambao wako madarakani wakati huu), akiwa na umri mdogo. Mwaka 1994, kabla ya kutokea kwa mauaji ya kimbari, Emile gafirita alikua katika kikosi kiliyokua kilipiga kambi wakati huo, katika majengo ya Bunge la zamani CND. Tangu mkataba wa amani wa Arusha, eneo hilo lilichukuliwa na waasi wa RPF kama makao yake makuu, mjini Kigali.

Katika barua aliyowaandikia majaji wa Ufaransa wanaofuatilia kesi ya hayati rais Juvenal Habyarimana, Emile Gafirita, alibaini kwamba alishiriki katika msafara wa magari ya waasi wa RPF yaliyobeba makombora yaliyotumiwa kwa kudungua ndege ya hayati rais Juvenal Habyarimana, hadi kwenye makao makuu ya waasi wa RPF, CND.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.