Pata taarifa kuu
DRC-BENI-ADF-Usalama

DRC: Usalama waendelea kudorora Beni

Watu wasiopungua kumi wakiwemo wafanyabiashara na viongozi wastaafu wa mjini Beni katika jimbo la Kivu Kaskazini wanadaiwa kukamatwa tangu siku ya Jumatano Novemba 19 na maafisa wa Usalama wa Taifa (ANR).

Mazishi ya mtu mmoja alieuawa katika shambulio liliyotokea katika kitongoji cha mji wa Beni, katika mkoa wa Kivu Kaskazini (DRC), Oktoba 21 mwaka 2014.
Mazishi ya mtu mmoja alieuawa katika shambulio liliyotokea katika kitongoji cha mji wa Beni, katika mkoa wa Kivu Kaskazini (DRC), Oktoba 21 mwaka 2014. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa waliokamatwa ni rais wa Shirikisho la Wamiliki wa makampuni nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FEC), tawi la Beni, Bi. Gertrude Vihumbira, meya wa zamani wa mji wa Beni Didier Paluku Kisaka, na wafanyabiashara wengine watano wa vitongoji vya Kasindi na Rwenzori.

Kamatakamata hiyo imeanza kuwajengea baadhi ya watu hofu ya hali ijayo mjini humo ambapo kwa taarifa zisizo rasmi, baadhi yao wakiwemo wafanyabiashara Kazebere na Jeannine Mambura tayari wamepelekwa jijini Kinshasa kujibu tuhuma zinazowakabili.

Juma lililopita, Gavana wa Mkoa wa Jimbo la Kivu Kaskazini Julien Paluku katika kikao na waandishi wa habari, alibainisha kuwepo kwa mpango wa uasi mpya nchini humo, chimbuko lake likiwa Eneo la Beni na kuwaonya watu kuhusu ushirikiano wa baadhi ya watu hao bila ya kutaja majina yao.

Shutuma za uhalifu wa makundi ya waasi wanaohatarisha hali ya usalama mkoani humo zimezungumziwa na serikali kutekelezwa na waasi wa ADF-Nalu, lakini hukumu ya hivi majuzi juu ya mauwaji ya Kanali Mamadou Ndala umebaini ushirikiano wa baadhi ya askari wa FARDC na waasi hao na kusababisha hali ya sintofahamu mjini Beni.

Hayo yakijiri mashirika ya kiraia wilayani Beni Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, yamesema raia katika Wilaya hiyo wanaendelea kuisihi kwa hofu kutokana na mdororo wa usalama unaoendelea kushuhudiwa katika eneo hilo.

Juma hili, msafara wa wanajeshi wa kulinda amani MONUSCO ulivamiwa katika eneo la Mavivi wilayani Beni na kuzua wasiwasi mkubwa katika eneo hilo ambalo limeendelea kushambuliwa na waasi wa ADF NALU.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.