Pata taarifa kuu

Unyanyasaji dhidi ya wanawake bado ni tishio

Novemba 25 ni siku ya kimataifa dhidi ya unyanyasaji kwa wanawake. Leo Jumanne Novemba 25 ulimwengu unaungana na wanawake kwa kupiga vita vitendo aina yoyote vinavyomdhalilisha mwanamke.  

Hopitali Heal Africa ya mjini Goma, jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Raia wa mashariki mwa Congo wamekua wakitoa taarifa kuhusu visa vya unyanyasaji dhidi ya wanawake.
Hopitali Heal Africa ya mjini Goma, jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Raia wa mashariki mwa Congo wamekua wakitoa taarifa kuhusu visa vya unyanyasaji dhidi ya wanawake. AFP PHOTO/Junior D. Kannah
Matangazo ya kibiashara

Vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana vimekithiri katika mataifa mbalimbali ulimwenguni, hasa barani Afrika. Wasichana wa mitaani Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, waathirika wa unyanyasaji wa majumbani nchini Afrika Kusini au tohara Cote d'Ivoire: barani Afrika, visa vya unyanyasaji ni vingi, lakini watu wamekua hawatowi taarifa kuhusu visa hivyo.

Wanawake wanaoishi katika maeneo yaliyokumbwa na mapigano ya muda mrefu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wanakakabiliwa na unyanyasaji husuan ubakaji, kupigwa na kudhalilishwa.

Hata hivo katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kinshasa, unyanyasaji dhidi ya wanawake pia ni tatizo kubwa. Zaidi ya watoto 20,000 wanakimbilia katika mji huo huku wengine wakiishi mitaani. Kulingana na takwimu ziliyotolewa na mashirika mbalimbali yanayotetea haki za binadamu mmoja kati ya watoto wawili wa mitaani mjini Kinshasa ni msichana.

Karibu asilimia 70 ya wasichana wa mitaani mara kwa mara wanabakwa na wananyanyaswa. Tangu mwaka 1999, shirika la madaktari wa ulimwengu walianzisha programu ya kusaidia wasichana hao na kuwaelimisha kuhusu vitendo hivyo.

Nchini Cote d'Ivoire, wanawake mara kwa mara wanakabiliwa na ukeketaji na kupigwa na waume zao.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.