Pata taarifa kuu
EU-DRC-MUKWEGE-Haki za wanawake-Jamii

Daktari Mukwege apewa rasmi tuzo Sakharov na Bunge la Ulaya

Baada ya miaka ya mapambano kwa wanawake waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Daktari Denis Mukwege amepokea tuzo ya kifahari ya Sakharov iliyotolewa na Bunge la Ulaya mjini Strasbourg, Mashariki mwa Ufaransa. Jumatano, Novemba 26 mwaka 2014.

Rais wa Bunge la Ulaya, Martin Schulz, amemsifu " mtu ambaye anapambana kwa kutetea wanawake nchini mwake", Daktari Denis Mukwege.
Rais wa Bunge la Ulaya, Martin Schulz, amemsifu " mtu ambaye anapambana kwa kutetea wanawake nchini mwake", Daktari Denis Mukwege. REUTERS/Vincent Kessler
Matangazo ya kibiashara

Wabunge wa Ulaya wamekaribishwa hotuba yake kwa vifijo na furaha. Hofu ya daktari Mukwege ni kuendelea kutambua matumizi ya ubakaji kama silaha ya vita.

β€œ Muili wa mwanamke umekua ni uwanja wa vita na unyanyasaji umnatumiwa kama silaha ya vita. Athari ni nyingi na madharani mengi katika jamii. Watu wamekua kama watumwa wa ngono, hali hii inasikitisha na inatia huzuni”, amasema Daktari Mukwege.

Denis Mukwege alianzisha hospitali ya Panzi mwaka 1998, katika mkoa wa Kivu Kaskazini ili kusaidia wanawake na wasichana wanaodhalalishwa kingono katika na baada ya vita viliyoikumba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa kipindi cha miaka ishirini.

Wanawake zaidi ya nusu milioni nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walibakwa tangu machafuko yalipozuka, huku wanawake 40,000 wakiwa wlipata huduma za matibabu katika hospitali ya Denis Mukwege.

Daktari Denis Mukwege raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anatambuliwa kimataifa katika juhudi zake za kutoa huduma za afya kwa wasichana na wanawake waliobakwa Mashariki mwa nchi hiyo.

Rais wa bunge hilo la Umoja wa Ulaya Martin Schulz amemwelezea Dakatri Mukwege kama mtu aliyetoa mchnago mkubwa kuwatetea wanawawake wanaobakwa.

Mukwege amesema tuzo hiyo itaendeleza mapambano ya kuendelea kuwasaidia wananwake wanaobakwa na kutetea haki zao Mashariki mwa nchi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.