Pata taarifa kuu
BURUNDI-BNUB-SIASA-USALAMA

BNUB yafunga milango yake Burundi

Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi BNUB imekamilisha shughuli zake nchini humo, baada ya miaka zadi ya 10 ikisimamia amani na kuchangia kurejesha usalama na maridhianao kati ya wanasiasa.

Agathon Rwasa, kiongozi wa kihistoria wa chama cha FNL, akizungukwa na wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Afrika kutoka Afrika Kusini, Bujumbura, Novemba 29 mwaka 2009.
Agathon Rwasa, kiongozi wa kihistoria wa chama cha FNL, akizungukwa na wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Afrika kutoka Afrika Kusini, Bujumbura, Novemba 29 mwaka 2009. AFP/Esdras Ndikumana
Matangazo ya kibiashara

Akisimamia sherehe hizo naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anaye husika na maswala ya siasa  Jeffrey Feltman ameisihi serikali pamoja na wanasiasa kuanda mazingira mazuri ya uchaguzi.

Ofisi hiyo ya Umoja wa Mataifa ilibadili jina pamoja na majukumu yake, ambapo awalii ilikua ikijulikana kwa jina la BUNUB, na ilikua ikijihusisha na kuwalindia usalama baadi ya wanasiasa ambao walikua wakitokea uhamishoni.

Wakati huo tume hiyo ya Umoja wa mataifa ilisaidia kwa kuboresha maridhianao kati ya wanasiasa na kurejesha hali ya utulivu nchini.

Hata hivyo Burundi bado inakabiliwa na changamoto za kiusalama, wakati ambapo imesalia miezi isiyozidi sita ili uchaguzi wa madiwani ufanyike.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inafunga milango yake nchini Burundi wakati ambapo mvutano bado unaendelea kati ya upinzani na tume huru ya uchaguzi kuhusu zoezi la kuandika wapiga kura.

Upinzani umekua ukiishtumu tume huru ya uchaguzi kupanga njama na chama tawala Cndd-Fdd ili waweze kuiba kura. Zoezi la kuandika wapiga kura limeingia dosari, na kupelekea upinzani kuiomba tume huru ya uchaguzi ijiuzulu.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa itarudiliwa na tume ya Umoja wa Mataifa itakayosimamia uchaguzi MENUB ambayo inatarajia kuanza shughuli yake mwanzoni mwa mwezi Jnuari mwaka 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.