Pata taarifa kuu
BURUNDI-RWASA-UPINZANI-FNL-SIASA-SHERIA

Rwasa arejea nyumbani bila kusikilizwa

Agathon Rwasa amerejea nyumbani kwake bila kusikilizwa na Mahakama, baada ya kuripoti Mahakamani Jumatano Desemba 15. 

Kiongozi wa kihisoria wa kundi la zamani la waasi la Palipehutu Fnl, Agathon Rwasa (katikati), akilindwa na waskari wa kikosi cha Umoja wa Afrika kutoka Afrika Kusini, Mei mwaka 2008.
Kiongozi wa kihisoria wa kundi la zamani la waasi la Palipehutu Fnl, Agathon Rwasa (katikati), akilindwa na waskari wa kikosi cha Umoja wa Afrika kutoka Afrika Kusini, Mei mwaka 2008. (Photo : AFP)
Matangazo ya kibiashara

Mahakama haikutoa taarifa kuhusu sasabu ziliyopelekea kiongozi huyo wa kihistoria wa kundi la zamani la waasi la Palipehutu-Fnl nchini Burundi kutosikilizwa.

Agathon Rwasa alipowasili Mahakami alipokelewa na mamia kwa maelfu ya wafuasi wake, huku kukionekana idadi kubwa ya askari polisi.

Methusela Nikobamye, aliye kuwa msemaji wa kundi la waasi la Palipehutu-Fnl, ambaye amekua ameripoti mahakamani, naye pia hakusikilizwa.

Kiongozi  huyo wa kihistoria wa kundi la zamani la waasi la Palipehutu-Fnl, ambalo lilianzasha vita vya maguguni katika miaka ya 1980 nchini Burundi, kabla ya kutia saini mkataba wa kudumu wa kusitisha mapigano katika mwaka wa 2006 ameripoti Mahakamani, baada ya aliye kuwa msemaji wa kundi hilo, Methusela Nikobamye, maarufu Pasteur Habimana kuitishwa mara kadha Mahakamani.

Agathon Rwasa,kiongozi wa kihistoria wa Fnl,  Novemba 29 mwaka 2009.
Agathon Rwasa,kiongozi wa kihistoria wa Fnl, Novemba 29 mwaka 2009. AFP/Esdras Ndikumana

Wawili hao wanakabiliwa na mashitaka ya mauaji ya wakimbizi raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutoka jamii ya Banyamulenge walioshambuliwa na wapiganaji wa kundi la Palipehutu-Fnl mwaka 2004 tarafani Gatumba karibu na mpaka wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Awali Methusela Nikobamye, aliye kuwa msemaji wa Palipehutu-Fnl alibaini kwamba anashangazwa na kuitishwa kwake Mahakamani ili kujibu tuhuma za mauaji ya raia wa kigeni kutoka Congo, wakati kesi kuhusi raia wa Burundi waliouawa katika vita viliyoisibu Burundi tangu mwaka 1993 hadi 2006 hazijawahi kusikilizwa na Mahakama za nchini humo.

Methusela Nikobamye alivikosoa vyombo vya sheria vya Burundi kwamba vinatumiwa na utawala wa chama cha Cndd-Fndd, ili kuwasambaratisha viongozi wa kundi la zamani la waasi la Palipehutu-Fnl, ambao walikataa kujiunga na chama tawala Cndd-Fdd, huku akibaini kwamba waasi kutoka makundi yote yaliyokua yakiendesha vita dhidi ya tawala ziliyotangulia, likiwemo kundi la waasi wa Cndd-fdd, walipewa msamaha wa muda hadi pale Mahakama maalumu ya Umoja wa Mataifa itakayoshughulikia kesi za mauaji yaliyotokea nchini Burundi katika ghasia ziliyotokea kati ya mwaka 1965 hadi mwaka 2006.

Aimé Magera, msemaji wa Agathon Rwasa (akiwa mbele ya gari na wanahabari) akimsabahi Agathon Rwasa (ndani ya gari), Agosti 6 mwaka 2013.
Aimé Magera, msemaji wa Agathon Rwasa (akiwa mbele ya gari na wanahabari) akimsabahi Agathon Rwasa (ndani ya gari), Agosti 6 mwaka 2013. AFP PHOTO/Esdras Ndikumana

Msemaji wa agathon Rwasa, Aimé Magera amesema kuwa vyombo vya sheria vya Burundi haviko huru na ndio maana utawala umekua ukivishawishi ili vimpotezee muda Agathon rwasa asiwezi gumbea kwenye uchaguzi ujao wa urais.

Itafahamika kwamba raia wa Congo kutoka jamii ya Banyamulenge waliwafungulia mashitaka viongozi hao wa zamani wa kundi la waasi la Palipehutu-Fnl mbele ya vyombo vya sheria vya kimataifa pamoja na vyombo vya sheria nchini Burundi.

Septemba mwaka  2006, rais wa Burundi Pierre Nkurunziza (kulia) akiwa pamoja na kiongozi wa kihistoria wachama cha FNL Agathon Rwasa, baada ya kusaini mkataba wa kutudumu wa amani mjini Dar es Salaam.
Septemba mwaka 2006, rais wa Burundi Pierre Nkurunziza (kulia) akiwa pamoja na kiongozi wa kihistoria wachama cha FNL Agathon Rwasa, baada ya kusaini mkataba wa kutudumu wa amani mjini Dar es Salaam. (Photo: AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.