Pata taarifa kuu
UN-SUDANI KUSINI-KIIR-MACHAR-USALAMA

UN yasikitishwa na machafuko yanayoendelea Sudani Kusini

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon amewashutumu rais wa Sudani Kusini Salva Kirr na kiongozi wa waasi Riek Machar kwamba wameendelea kuweka mbele maslahi yao kwa kuhatarisha usalama wa raia.

Wakimbvizi wa ndani 17,000 wa Sudani Kusini, ambao wanapewa hifadhi katika kambi ya Umoja wa Mataifa iliyojengwa katika kituo cha Umoja wa mataifa mjini Juba, Januari 10 mwaka.2014.
Wakimbvizi wa ndani 17,000 wa Sudani Kusini, ambao wanapewa hifadhi katika kambi ya Umoja wa Mataifa iliyojengwa katika kituo cha Umoja wa mataifa mjini Juba, Januari 10 mwaka.2014. Reuters/Andreea Campeanu
Matangazo ya kibiashara

Baada ya mwaka mmoja vita kati ya marafiki hao hasimu kuanza tena nchini Sudan Kusini, Katibu mkuu wa umoja wa mataifa, amesema mgogoro kati ya mahasimu wakuu wawili wa taifa hilo ndio unaosababisha taifa hilo kuendelea katika dimbwi la machafuko.

Ban Ki-moon amesema kwamba kushindwa kufikia makubalianao kati ya pande hizo mbili kumeendelea kuhatarisha maisha ya mamilioni ya watu, huku akisikitishwa kuona malengo yaliyowaweka pamoja wawili hao na viongozi ambao kwa sasa ni marehemu wakati wa kutetea uhuru wa Sudani Kusini yamevunjika.

Mapigano kati ya makundi hasimu tiifu kwa Rais Salva Kiir na yale yanayomuunga mkono makamu wa zamani wa Rais Riek Machar, yamesambaratisha kabisa miji mikuu muhimu Nchini humo.

Machafuko yanayoendelea kushuhudiwa katika taifa changa la Sudani Kusini yamesababisha vifo vya maefu ya raia, huku watu zaidi milioni moja wakiyahama makaazi yao.

Nchi jirani pamoja na Jumuiya ya maendeleo ya Afrika Mashariki vilitahidi kuingilia kati kwa kusuluhisha pande hizo mbili bila mafaniko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.