Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-MANDELA-WINNIE-MACHEL-SHERIA-HAKI

Winnie Mandela akataliwa kumiliki mali ya Mandela

Winnie Mandela, aliye kuwa mke wa rais wa zamani wa Afrika Kusini, hayati Nelson mandela Madiba, amekataliwa kurithi mali ya aliye kuwa mumewe, kama walivyobainisha wanahusika na kugawa mirathi wa rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini. 

Winnie Mandela, aliye kuwa mke wa Nelson Mandela Madiba, hapa ni Oktoba 30 mwaka 2014, akikataliwa kpewa umiliki wa makazi ya Qunu.
Winnie Mandela, aliye kuwa mke wa Nelson Mandela Madiba, hapa ni Oktoba 30 mwaka 2014, akikataliwa kpewa umiliki wa makazi ya Qunu. AFP PHOTO/GIANLUIGI GUERCIA
Matangazo ya kibiashara

Kwa kipindi cha miezi miwili, Winnie Mandela, amekua akijaribu kupata milki ya makazi ya Nelson Mandela katika kijiji kidogo cha Qunu, bila mafanikio.

Watu hao wanahusika na kugawa mirathi ya Nelson Mandela, wamebaini kwamba watapinga kwa vyovyote vile ombi la Winnie Mandela, la kutaka apate umiliki wa makazi hayo.

Winnie Mandela, aliishi na Mandela katika ndoa kwa kipindi cha miaka 38 , lakini hakuwekwa kwenye orodha ya watu wanaopaswa kupewa mirathi ya rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini. Leo, Winnie Mandela, anadhani kuwa makazi ya Qunu ni milki yake, kwani Mandela aliipata wakiwa pamoja katika ndoa.

Winnie Mandela, amefungua mashitaka kwenye Korti kuu ya Mthatha, nchini Afrika Kusini.

Hata hivyo wanaohusika na kugawa mirathi ya Nelson Mandela, wamesema katukatu kwamba makazi ya Qunu ni milki ya mke wa tatu wa Nelson andela Madiba, Graça Machel. Jaribio lolote la marekebisho ya maandiko ya Nelson mandela ni kinyume na kauli yake. Licha ya kukosolewa, Winnie Mandela, ameendelea kuonesha kuwa yeye ndiye mwenye haki ya kumiliki mali ya Mandela, hususan makazi yake ya Qunu.

Winnie Mandela alikosoa vikali kwa nini Nelson Mandela alimpa Graça Machel makazi ya Qunu, wakati ambapo ana nusu ya uraia wa Msumbiji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.