Pata taarifa kuu
MADAGASCAR-RAVALOMANANA-Siasa-Usalama

Rais wa Madagascar akutana na Ravalomanana

Rais wa zamani wa Madagascar, ambaye amewekwa chini ya ulinzi tangu aliporejea nchini akitokea uhamishoni, ametembelewa Jumatatu Desemba 15 na rais wa sasa wa Madagascar, Herry Rajaonarimampianina.

Rais wa Madagascar, Hery Rajaonarimampianina, Januari mwaka 2014.
Rais wa Madagascar, Hery Rajaonarimampianina, Januari mwaka 2014. AFP PHOTO/RIJASOLO
Matangazo ya kibiashara

Ni mara ya kwanza wawili hao kukutana tangu Marc Ravalomanana kurudi nchini akitokea uhamishoni mwezi Oktoba mwaka 2014.

Ravalomanana na Rajaonarimampianina wamekutana katika kisiwa cha Nosy Be, si mbali na Diego Suarez, ambapo rais wa zamani anazuiliwa tangu miezi miwili iliyopita.

Mkutano huo ambao “ulipangwa tangu siku kadhaa”, umefanyika kwa siri, kwa mujibu wa rais wa Madascar, ambaye amethibitisha Jumanne Desemba 16, baada ya taarifa hiyo kuchapishwa kawenye magazeti siku moja kabla.

“ Je nilikutana na Ravalomanana, jibu ni ndio. Nilifanya hivyo kwa lengo la maridhiano ya kitaifa”, amesema rais wa Madagascar, Rajaonarimampianina.

Alipohojiwa iwapo rais Ravalomanana, ataachiliwa huru kabla ya siku kuu za mwisho wa mwaka, rais Rajaonarimampianina, amejibu akiwataka raia wasiwe na haraka, akibaini kwamba wameanzisha mchakato huo.

Ndugu jamaa na wafuasi wa Ravalomanana wamethibitisha hata hivyo kwamba mkutano ulikua mzuri, huku wengine wakibaini kwamba huenda kuna mkataba ambao umefikiwa, na huenda rais huyo wa zamani akaachiliwa huru hivi karibuni, aidha akahamishwa na kuletwa karibu na familia yake

Ndugu jamaa na wafuasi wa Ravalomanana wamethibitisha hata hivyo kwamba mkutano ulikua mzuri, huku wengine wakibaini kwamba huenda kuna mkataba amabo umefikiwa, na huenda rais huyo wa zamani akaachiliwa huru hivi karibuni, aidha akahamishwa na kuletwa karibu na familia yake

Watu watano wanaohusishwa kupanga njama na Marc Ravalomanana wanaendelea kusalia kizuizini katika jela la Diego kwa kusubiri uamzi wa Mahakama. Watu hao ni mlinzi wa Marc Ravalomanana, Marc Koumba na maafisa wanne wa idara ya usafiri wa anga, ambao wanatuhumiwa kumsaidi rais huyo wa zamani kuingia nchini kinyume cha sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.