Pata taarifa kuu
KENYA-BUNGE-USALAMA

Muswada wa sheria waibua vurugu Bungeni

Hali ya sintofahamu imetokea katika Bunge la Kenya Alhamisi Desemba 18 wakati wabunge walikua wakijiandaa kujadili muswada wa sheria kuhusu usalama, ambapo baadhi ya wabunge walionekana wakipigana makonde na kuzuia shughuli za Bunge kuendelea.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta. Reuters/Noor Khamis
Matangazo ya kibiashara

Wabunge kutoka muungano wa vyama vya upinzani CORD wamefanikisha azma yao ya kuzua ghasia na kuvuruga shughuli Bungeni baada ya kubainika kua Bunge litajadili aidha kupitisha au kufutilia mbali muswada kuhusu usalama.

Wabunge kutoka muungano wa vyama vya upinzani wameikosoa hatua ya serikali ya kuwaweka maofisa wa usalama nje ya majengo ya Bunge, huku wakidai kuwa ilikua njama za kuwatishia usalama wao.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.