Pata taarifa kuu
MADAGASCAR--Siasa-Maridhiano

Marais wa Madagascar wakutana kwa maridhiano ya kitaifa

Marais wa zamani wanne na rais wa sasa wa Madagasar wanatazamiwa kukutana Ijumaa Desemba 19 katika mji wa Ivato pembezuni mwa mji wa Antananarivo kwa kwa lengo la kuboresha maridhiano ya kitaifa. Watano hao wanakutana katika mkutano wa faragha.

Marc ravalomanana, ambaye yuko chini ya ulinzi tangu aliporudi, akitokea uhamishoni miezi miwili iliyopita, anashiriki mkutano kuhusu mchakato wa maridhiano.
Marc ravalomanana, ambaye yuko chini ya ulinzi tangu aliporudi, akitokea uhamishoni miezi miwili iliyopita, anashiriki mkutano kuhusu mchakato wa maridhiano. AFP PHOTO/RIJASOLO
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo, ambao ulikua unasubiriwa kwa hamu na gamu, ni wa kihistoria, kwani ni kwa mara ya kwanza unafanyika, baada ya kujitokeza uhasama kati ya baadhi ya viongozi waliotawala nchini hiyo.

Taarifa ya mkutano huo imetangazwa na Ikulu ya Antananarivo na kamati ya maandalizi FFKM, ambayo ni Baraza la Kanisa Katoliki nchini Madagascar.

Didier Ratsiraka, Albert Zafy, Marc Ravalomanana, Andry Rajoelina na rais wa sasa Herry Rajaonarimampianina wataketi kwenye meza moja ya mazungumzo kutekeleza mchakato wa maridhiano ya kitaifa.

Kuleta watu hawa watano kwenye meza moja ni changamoto ya kwanza kuweka wazi kuwa mchakato wa maridhiano unawezekana, licha ya kuweko kwa kipindi kadhaa hali ya kutoelewana kati ya marais wa zamani Marc Ravalomanana na Andry Rajoelina. Hata hivyo mvutano huenda ukajitokeza kati ya wahusika.

Marais hao watano wanatazamiwa kushiriki mkutano huo, ikiwa ni pamoja na Marc Ravalomanana ambaye yuko chini ya ulinzi tangu aliporudi kutoka uhamishoni miezi miwili iliyopita. Andry Rajoelina pia anatazamiwa kuhudhuria mkutano huo, ingawa bado anasita kwa mchakato huo.

Hata hivyo Alhamisi Desemba 18 usiku watu watano waliotuhumiwa kumsaidia Marc Ravalomanana kuingia nchini humo kinyume cha sheria, wameachiliwa. Jean-Marc Koumba, mlinzi wa zamani wa rais wa zamani Marc Ravalomanana na raia wanne, ambao ni maafisa wa idara ya usafiri wa anga. Watano hao walikuwa kizuizini kwa miezi miwili katika jela la Diego Suarez.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.