Pata taarifa kuu
LIBYA-Mapigano-Usalama

Moto washambulia vituo vya mafuta Libya

Moto uliosababishwa na mapigano kati ya vikosi vya serikali na wanamgambo wa kiislam katika moja ya vituo vikubwa vya mafuta nchini Libya umeenea katika ghala zingine za mafuta. Mashahidi  wamebaini kuwa imekua vigumu kudhibiti hali hiyo.

Moto wateketeza kituo cha mafuta cha Al-Sedra Desemba 26. Kwa sasa ni vituo 5 ambavyo vinawaka moto.
Moto wateketeza kituo cha mafuta cha Al-Sedra Desemba 26. Kwa sasa ni vituo 5 ambavyo vinawaka moto. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Vurugu ziliendelea kushika kasi wiki iliyopita, mashariki mwa Libya. Wanamgambo wa Kiislam walishambuliwa vituo vya mafuta.

Wanajeshi 22 wa Libya waliuawa na kituo cha mafuta cha Al-Sedra kikachomwa moto. Kikuo hicho kinakaribiana na vituo vigine vya mafuta vya Ras Lanuf na Brega.

Uzalishaji wa mafuta nchini Libya umefikia sasa kwenye kiwango cha mapipa 350,000 kwa siku dhidi 800,000 kabla ya mapigano yaliozuka katikati ya mwezi Desemba. Kwa mujibu wa Sébille-Philippe Lopez, wa kampuni ya utafiti Géopolia, Libya imepoteza nafasi yake kama mzalishaji kuu wa mafuta kwa muda mrefu ...

Wakati huo huo vikosi vya Libya, kwa mara ya kwanza viliendesha mashambulizi Jumapili Desemba 28 dhidi ya ngome za wapiganaji wa kiislam katika mji wa Misrata ambako walianzisha harakati zao za kuuteka mji mkuu wa Libya, Tripoli.

Mashambulizi haya ya angani dhidi ya mji wa tatu kwa ukubwa, kwenye umbali wa kilomita 200 mashariki mwa Tripoli, ni ya kwanza tangu kuanguka kwa utawala wa Muammar Gaddafi mwaka 2011 na mwanzo wa mapigamo ya kuwania madaraka ambayo yalitumbukiza Libya katika dimbwi la machafuko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.