Pata taarifa kuu
SENEGAL-WADE-HAKI-SHERIA

Uamzi watazamiwa kutolewa kufuatia ombi la Karim Wade

Haijafahamika iwapo Karim wade, mwanaye Abdoulaye Wade ataachiliwa huru kwa dhamana, wakati ambapo uamzi wa majaji ukisubiriwa kutolewa leo Jumatatu Desemba 28 mwaka 2014.

Karim Wade, mwana wa rais wa zamani wa Senegal atuhumiwa kujitajirisha kinyume cha sheria.
Karim Wade, mwana wa rais wa zamani wa Senegal atuhumiwa kujitajirisha kinyume cha sheria. AFP PHOTO / GEORGES GOBET
Matangazo ya kibiashara

Miezi sita baada ya kuanza kwa kesi ya Karim Wade, wanasheria wake waliwasilisha ombi mbele ya Mahakama Desemba 22 la kutaka mteja wao aachiliwe huru kwa dhamana dhidi ya ombi la Ofisi ya Mashitaka kutaka Karim Wade asalie jela.

Kesi hiyo inaendelea, lakini Karim Wade hawezi kukaa kwa muda usiojulikana kizuizini. Karim Wade tayari amesha kaa kizuizini kwa muda wa miezi 20. Hizo ni hoja zinazotolewa na mawakili wake.

Wiki iliyopita, Upande wa utetezi uliomba Mahakama inayoshughulikia kesi za kujitajirisha kinyume cha sheria kumuachilia huru kwa dhamana mteja wao.

Ombi hilo la kuachiliwa huru kwa dhamana Karim wade limepingwa na Ofisi ya Mashitaka, ikibaini kwamba ina hofu huenda akaondoka nchini baada ya kuachiliwa huru.

Ofisi ya Mashitaka imebaini pia kwamba kumuachilia huru Karim Wade, huenda akawapa hongo mashahidi.

Waziri wa zamani si peke yake kudai kuachiliwa huru kwa dhamana. Mshtakiwa wa pili, Mamadou Pouye ambaye anatuhumiwa kushirikiana na Karim Wade katika kashfa hiyo yuko kizuizini kwa zaidi ya siku 600.

Kama Karim Wade, wanasheria wa Mamadou Pouye wamebaini kwamba mteja wao anadhulumiwa haki zake wakati ambapo bado hajakabiliwa na hatia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.