Pata taarifa kuu
SENEGAL-WADE-HAKI-SHERIA

Mahakama inayomsikiliza Karim Wade yakosolewa

Mahakama inayoshughulikia kesi za kujitarisha kinyume cha sheria nchini Senegal, imeendelea kukosolewa katika kesi ya Karim wade, mwanae rais wa zamani wa Senegal, Abdoulaye Wade.

Karim Wade, mtoto wa rais wa zamani wa Senegal, akituhumiwa kujitajirisha kinyume cha sheria.
Karim Wade, mtoto wa rais wa zamani wa Senegal, akituhumiwa kujitajirisha kinyume cha sheria. AFP PHOTO / STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Jana, Jumatatu Desemba 29 bodi ya majaji wanaofuatilia kesi hiyo, ilikataa kutekeleza ombi la Karimu Wade la kumuachilia huru kwa dhama . Upande wa serikali, wamethibitisha kwamba vyombo vya sheria vinafanya kazi yake vikiwa huru. Lakini upinzani pamoja na baadhi ya viongozi wa mashirika ya kiraia wamebaini kuwa kesi hiyo ni ya kisiasa.

Hakuna mshangao katika jamii ya wanasiasa nchini Senegal. " Tulitarajia uamuzi kama huo", amesema Babacar Gaye, msemaji wa PDS, chama kikuu cha upinzani nchini Senegal.

Kwa upande wake, Mahakama inayoshughulikia kesi za kujitajirisha kinyume cha sheria, imebaini kwamba kuachiliwa huru kwa Karim Wade kunaweza kuhatarisha usalama wa wananchi. Hoja ambayo imetupiliwa mbali na Babacar Gaye.

Kwa mujibu wa Babacar Gaye, wananchi wanadai kuachiliwa huru kwa waziri wa zamani. Badala yake kuendelea kuzuiliwa Karim Wade kunaweza kuhatarisha usalama wa wananchi, amesema Babacar Gaye.

Katika safu ya chama cha RPA, chama cha rais Macky Sall, uamzi huo wa Mahakama umeibua hisia tofauti. Kwa mujibu wa Mbunge Sheikh Dionne, Karim Wade hapaswi kubaki katika jela. Kwa upande wake, Seydou Gueye, msemaji wa RPA, amethibitisha kuwa vyombo vya sheria viko huru.

" Kesi hiyo iko katika awamu ya kusikilizwa. Kama kuna baadhi ya ambao hawakufurahia uamzi huu, kuna njia zingine ambazo wanaweza kutumia", amesema Seydou Gueye.

Wanasheria wa Karim Wade wameamua kufikisha malalamiko yao mbele ya Koti kuu ili kujaribu kufuta uamzi uliochukuliwa na bodi ya majaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.