Pata taarifa kuu
BURUNDI-CIBITOKE-MAPIGANO-USALAMA

Mapigano Kaskazini Magharibi mwa Burundi

Mapigano yameendelea kwa siku ya pili kmkoani Cibitoke, Kaskazini Magharibi mwa Burundi karibu na mpaka na jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Burundi imekua na imani na jeshi lake kutokana na uzoefu wa jeshi hilo.
Burundi imekua na imani na jeshi lake kutokana na uzoefu wa jeshi hilo. AFP PHOTO / SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo ambayo ni kati ya waasi na jeshi yamesababisha hadi sasa vifo vya waasi 34 na mwanajeshi mmoja, kwa mujibu wa chanzo cha kijeshi.

Hakuna kundi hata moja ambalo limedai kuhusika katika mapigano hayo. Waasi hao walitokea Mashariki mwa Congo na kuingia Burundi baada ya kuvuka mto Rusizi.

Mapema Jumatano Desemba 30, mkuu wa mkoa wa Cibitoke, Anselme Nsabimana, alibaini kwamba waasi 14 waliuawa katika mapiganao hayo, huku baadhi yao wakikamatwa.

Mikoa ya Cibitoke (Kaskazini Magharibi) na Bubanza (Magharibi), imekua ikishambuliwa na makundi ya watu wenye silaha.

Miezi ya hivi karibuni, jeshi la Burundi lilikiri kuingia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ili kukabiliana na makundi ya watu wenye silaha ambayo yamekua yakiingia Burundi, na kuhatarisha usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.