Pata taarifa kuu
TANZANIA-MWAKA 2015-USALAMA-UCHUMI-SIASA-MAZINGIRA

Jakaya Kikwete: “ 2015 ni mwaka wa mwisho kwa kuiongoza Tanzania"

Katika hotuba yake ya kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015, rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amebaini wazi kwamba 2015 ni mwaka wa mwisho kwake kwa kuliongoza taifa la Tanzania.

Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete
Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete TZ govt
Matangazo ya kibiashara

“ Hizi ni salamu zangu za mwisho za mwaka mpya kutoa, nikiwa rais wa nchi yetu. Mwakani salamu kama hizi zitatolewa na rais wetu mpya. Mimi wakati huo nitakuwa raia wa kawaida kijijini kwangu Msoga nikifuatilia kwenye televisheni na radio hotuba ya rais wa awamu ya tano ya uongozi wa nchi yetu akitoa salamu zake za kwanza za mwaka mpya, itakuwa siku ya furaha na faraja kubwa kwangu”, amesema Jakaya Mrisho Kikwete.

Rais Kikwete amesema mwaka 2014 umemalizika kwa salama na amani, mipaka ya nchi ikiwa salama na hakuna tishio lolote la kiusalama kutoka ndani au nje ya nchi ya Tanzania, huku akibaini kwamba uhusiano wa Tanzania na nchi jirani na nyinginezo duniani ni mzuri.

“ Hakuna nchi iliyo adui au tunayoitilia shaka kuwa na njama za kuhatarisha usalama wa Tanzania. Nawapongeza wanadiplomasia wetu pamoja na viongozi na watendaji wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuendelea kuifanya nchi yetu kuwa salama”, ameongeza rais Kikwete.

Rais Kikwete amesema, Kulingana na taarifa za polisi, mwaka 2014 vitendo vya uhalifu vimepungua ikilinganishwa na mwaka 2013. Mwaka 2014, matukio ya uhalifu yaliyoripotiwa polisi yalikuwa 64,088 ikilinganishwa na matukio 66,906 katika mwaka 2013.

“ Haya ni matokeo ya kazi nzuri inayofanywa na Jeshi la Polisi wakishirikiana na vyombo vingine vya usalama pamoja na raia wema. Naomba ushirikiano huu uendelee mwaka ujao na miaka ijayo ili tuweze kupata mafanikio makubwa zaidi”.

Rais Kikwete amepongeza kazi kubwa inayofanywa na polisi wa barabarani akisema kwamba matukio ya ajali za barabarani nchini yameendelea kupungua. Mwaka 2014 kumetokea ajali 14,048 zilizosababisha vifo vya watu 3,534 na wengine 16,166 kujeruhiwa. Mwaka 2013 kulitokea ajali 22,383 zilizosababisha vifo 3,746 na majeruhi 19,433. Hivyo mwaka huu kulikuwa na ajali 8,335, vifo 212 na majeruhi 3,267 pungufu kuliko mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.