Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAREKANI-KATIBA-SIASA-USALAMA

Rais Nkurunziza aonywa kutogombea muhula wa tatu

Mjumbe maalum wa Marekani katika ukanda wa Maziwa Makuu, Russ Feingold amesema kuwa rais Pierre Nkurunziza wa Burundi hapaswi tena kugombea awamu ya tatu ya urais nchini humo.

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza.
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza. Reuters / Alessandro Di Meo
Matangazo ya kibiashara

Russ Feingold, mjumbe maalum wa Marekani katika ukanda wa Maziwa Makuu.
Russ Feingold, mjumbe maalum wa Marekani katika ukanda wa Maziwa Makuu. AFP/Saul Loeb

Feingold ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari ambapo amesisitiza pia kuwa shughuli za kijeshi dhidi ya waasi wa zamani wa Rwanda wa FDLR lazima zianze ifikapo tarehe 2 mwezi Januari kufwatia makataa yaliyotolewa na jumuiya ya ICGLR na SADC.

Burundi siyo nchi pekee kupata aina hii ya ujumbe wa Marekani, tayari Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya ukanda wa Maziwa Makuu kutoa wito kwa Rais Kabila wa Congo na rais Kagame wa Rwanda, kuheshimu katiba za nchi zao husika.

Rais Pierre Nkurunziza kwa kiasi kikubwa anatarajiwa kugombea kwa muhula wa tatu na kuzidisha mihula miwili ambayo inaruhusiwa na katiba ya taifa hilo.

Akiwa ziarani mjini Bujumbura katikati ya mwaka 2014, balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Samantha Power, aliwataka viogozi wa Burundi kuheshimu uhuru wa kisiasa, na vilevile kuheshimu Katiba ya nchi, ambayo utawala ulikua ukijaribu kuifanyiya marekebisho ili kumpa nafasi rais Nkurunziza aweze kugombea mhula wa tatu, bila mafanikio.

“ Tunasisitiza kuheshimu katiba ya nchi, ambayo ni sheria mama ya Burundi, na vilevile kuheshimu haki za binadamu,” alisema Samantha Power baada ya mazungumzo na rais Pierre Nkurunziza.

Baada ya Bunge kutoidhinisha rasimu ya marekebisho ya katiba Mwezi Machi mwaka 2014, ambayo ingelimpa nafasi rais wa Burundi Peirre Nkurunziza kugombea muhula wa tatu, baada ya kugombea mihula miwili (2005-2010 na 2010-2015), Waziri wa mambo ya ndani, Edouard Nduwimana,alibaini kwamba hatua hiyo ya Bunge haimkatazi rais Pierre Nkurunziza kugombea kwa mara nyingine tena kiti cha urais katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Waziri Edouard Nduwimana aliyasema hayo katika kikao na viongozi wa dini mwaka 2014.

Tangazo hilo la waziri Nduwimana lilizua tafrani na utata baina ya wanasiasa na vyama vya kiraia nchini Burundi.

“ Haya ninayasema, kutokana na kwamba kuna watu ambao wamekua wakifikiria kwamba rais Nkurunziza hawezi kugombea muhula mwengine, si kweli”, alisema Waziri Nduwimana.

“ Ninawasihi wanasiasa ambao watagombea kwenye kiti cha urais, wajiandae wakijua kwamba watagombea kwenye nafasi hio pamoja na rais alie madarakani sasa", aliendelea kusema Edouard Nduwimana.

Wakati huo chama tawala cha CNDD-FDD, kupitia msemaji wake Onesime Nduwimana, kilisema bado hakijakutana ili kiamuwe atakayegombea kwa tiketi yake kwenye kiti cha urais katika chaguzi za 2015.

John Kerry (kulia), Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, akiwa pamoja na rais wa Burundi Pierre Nkurunziza (kushoto), Jumatatu Agost 4 mwaka 2014, mjini Washington.
John Kerry (kulia), Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, akiwa pamoja na rais wa Burundi Pierre Nkurunziza (kushoto), Jumatatu Agost 4 mwaka 2014, mjini Washington. REUTERS/Yuri Gripas

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.