Pata taarifa kuu
GAMBIA-MAPINDUZI-SIASA

Jammeh ayatuhumu mataifa ya kigeni

Siku mbili baada ya jaribio la mapinduzi kufeli nchini Gambia, rais wa nchi hiyo Yahya Jammeh amekanusha kuhusika kwa jeshi na kuyatuhumu mataifa ya kigeni yenye nguvu kuhusika katika kile alichotaja shambulio.

Rais wa Gambia Yahya Jammeh (hapa ilikua mwaka 2011) alikuwa nje ya nchi wakati jaribio la mapinduzi lilifanyika Jumanne Desemba 30 mwaka 2014.
Rais wa Gambia Yahya Jammeh (hapa ilikua mwaka 2011) alikuwa nje ya nchi wakati jaribio la mapinduzi lilifanyika Jumanne Desemba 30 mwaka 2014. AFP PHOTO / SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

Rais Yahya Jammeh ameyasema hayo katika hutoba kwa taifa aliyotoa Alhamisi Januari 1 mwaka 2015, akiukaribisha mwaka mpya wa 2015.

Rais huyo wa Gambia amewaonya " wale wanaotaka mabadiliko ya utawala kupitia ghasia". Raia wengi na awanajeshi wamekamatwa.

Hii ni kwa mara ya pili, rais Yahya Jammeh kuwahutubia wananchi wake tangu lilipofeli jaribio la mapinduzi.

Amesema jaribio la mapinduzi lililofeli Jumanne ni shambulio lililoendeshwa na "kundi la kigaidi linaloungwa mkono na mataifa ya kigeni yenye nguvu", ambalo linaundwa na wapinzani waishio Marekani, Ujerumani na Uingereza. " Baadhi ya silaha zao zilitengenezwa Marekani", amesema rais Yahya Jammeh.

Hata hivyo Marekani imekanusha kuhusika katika jaribio hilo la mapinduzi nchini Gambia

Kwa mujibu wa afisa wa jeshi, washambuliaji walikuwa wakiongozwa na afisa wa zamani katika jeshi aliyetoroka aitwaye Lamin Sanneh, ambaye aliuawa katika mapigano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.