Pata taarifa kuu
KENYA-UGAIDI-USALAMA

Sheria mpya za usalama: uamzi wa Mahakama watazamiwa kutolewa

Mahakama kuu jijini Nairobi nchini Kenya, leo Ijumaa Januari 1 itatoa uamuzi ikiwa sheria mpya za usalama nchini humo zisitishwe au ziendelee kutumiwa wakati kesi iliyowasiliwa na wanasiasa wa upinzani na Mashirika ya kiraia ikiendelea kusikilizwa.

Askari polisi wakipiga doria ili kuimarisha usalama Kanisani na Miskitini pamoja na maeneo muhimu yanayotembelea na watu wengi mjini Nairobi.
Askari polisi wakipiga doria ili kuimarisha usalama Kanisani na Miskitini pamoja na maeneo muhimu yanayotembelea na watu wengi mjini Nairobi. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Muungano wa upinzani CORD na Mashirika ya kiraia, yalikwenda Mahakamani kutaka sheria hizo mpya za usalama kusitishwa kwa madai kuwa zinakiuka haki za binadamu na kwenda kinyume na Katiba ya nchi hiyo.

Serikali imesema sheria hizo mpya zilizopitishwa na Bunge zitasaidia kupambana na ugaidi kutokana na Kenya kuendelea kupata vitisho kutoka kwa kundi la Al Shabab nchini Somalia.

Kifungo kinacholeta utata kuhusu sheria hiyo ni pamoja na mshukiwa wa ugaidi kuzuiliwa kwa kipindi cha mwaka mmoja bila kupelekwa Mahakamani na wanahabari kupata idhini ya polisi kabla ya kuchapisha habari au picha kuhusu matukio ya ugaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.