Pata taarifa kuu
Soka Barani Afrika-Can 2015

AFCON 2015: Tunisia na Cape-Verde zatoka sare

Michuano ya Kombea la mataifa ya Afrika yaliingia siku yake ya pili hiyo jana Jumapili Januari 18, ambapo katika mechi ya kwanza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Zambia wamejitupa uwanjani.

Mchezaji wa Cape-Verde, Nuno Rocha (kushoto) akipambana na Yassine Chikhaoui, kiongo wa Tunisia, Jumapili Januari 18 mwaka 2015 katika uwanja wa Ebebiyin.
Mchezaji wa Cape-Verde, Nuno Rocha (kushoto) akipambana na Yassine Chikhaoui, kiongo wa Tunisia, Jumapili Januari 18 mwaka 2015 katika uwanja wa Ebebiyin. AFP PHOTO / KHALED DESOUKI
Matangazo ya kibiashara

Hadi dakika tisini za mchezo timu hizo zilijikuta zikitoka sare ya kufungana bao 1-1. hata hivyo Zambia ambayo ilianza kuliona lango la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ilishindwa kutawala mchezo, hadi kujikuta inapashikwa bao la kusawazisha katika kipindi cha pili cha mchezo, bao lililowekwa kimyani na Yannick Bolasie.

Mechi ya pili ilizikutanisha Tunisia na Cape-Verde ambazo zote zikiwa katika kundi B. Mechi hiyo pamoja na ile iliyozikutanisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Zambia zilichezwa katika uwanja wa Ebebiyin.

Tunisia ambayo imekua ikipewa nafasi kubwa ya kuongoza katika kundi B, imeshindwa kufanya vizuri katika mechi yake na Cape-Verde. Hadi kipenga cha mwisho timu zote hizo mbili zilijikuta zikitoka sare ya kufungana bao 1-1.

Katika michuano yote iliyozikutanisha timu za kundi B hapo jana Jumapili, hakukuweko na mshindi, kama ilivyokuwa katika michuano iliyotangulia Jumamosi Januari 17, ambapo baada ya Congo na Equatorial Guinea kutoka sare, Gabon iliiburuza Burkina Faso, na kuwa timu ambayo inaongoza katika kundi A.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.