Pata taarifa kuu
Tanzania

Rais wa Tanzania afanya mabadiliko katika baraza la mawaziri

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho kikwete amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri ambapo amewateua mawaziri wapya wanane pamoja na manaibu watano. 

Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete
Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete TZ govt
Matangazo ya kibiashara

Akitangaza mabadiliko hayo Katibu mkuu koingozi balozi Ombeni Sefue katika ikulu ya rais jijini Dar es Salaam, Balozi Sefue amewataja mawaziri wapya walioteuliwa katika nafasi mbalimbali na wengine kuhamishwa katika nafasi zao za awali.

Mabadiliko hayo yanajumuisha wadhifa wa aliyekuwa waziri wa nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo ambaye amejiuzulu jana Jumamosi pamoja na wadhifa wa aliyekuwa waziri wa ardhi nyumba na makazi ambao uliachwa wazi na Profesa Anna Tibaijuka.

Mawaziri hao wawili wanahusishwa na kashfa ya ufisadi ambayo ilimshinikiza mwanasheria mkuu wa serikali ya hiyo pia kujiuzulu.
Nafasi ya Profesa Muhongo imechukuliwa na aliyekuwa naibu waziri wa ardhi, George Simbachawene.

Rais Kikwete amewaapisha mawaziri hao wapya hiyo jana katika tangazo lililorushwa hewani moja kwa moja na runinga ya taifa
Yafuatayo ni baadhi ya majina ya mawaziri walioteuliwa na wengine kuhamishwa nafasi zao.

Walioteuliwa katika nafasi ya uwaziri ni pamoja na George Simachawene waziri wa nishati na madini
Mary Nagu- waziri wa nchi [afisi ya rais] mahusiano na uratibu
Christopher chiza -waziri uwezeshaji na uwekezaji
Harisson Mwakyembe[waziri wa ushirikiano wa afrika mashariki]
William Lukuvi -waziri wa ardhi nyumba na makaazi
Steven Wasira -waziri wa kilimo chakula na ushirika
Samwel Sita -waziri wa uchukuzi
Jenista Muhagama -waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera uratibu na bunge

Manaibu waziri ni Stephen Masele -naibu waziri afisi ya makamu wa rais muungano
Angela Kariuki -naibu waziri wa ardhi nyumba na makaazi
Ummi Mwalimu- naibu waziri wa katiba na sheria
Anna Kilango naibu waziri wa elimu na mafunzo ya kiufundi
Charles Mwijage-naibu waziri wa nishati na madini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.