Pata taarifa kuu
MISRI-MAANDAMANO-VIFO-USALAMA

Watu zaidi ya 20 wamefariki Misri

Watu zaidu ya Ishirini wamepoteza maisha nchini Misri baada ya Makabiliano kati ya polisi na waandamanaji.

Waandamanaji wanaoipinga serikali ya Misri baada ya makabiliano ya vurugu na waandamanaji wanaounga mkono serikali. Cairo, Januari 25 mwaka 2014.
Waandamanaji wanaoipinga serikali ya Misri baada ya makabiliano ya vurugu na waandamanaji wanaounga mkono serikali. Cairo, Januari 25 mwaka 2014. REUTERS/Asmaa Waguih
Matangazo ya kibiashara

Maafisa watatu wa polisi ni miongoni mwa waliopoteza maisha, wakati wa maandamano hayo ya kuadhimisha miaka minne tangu kuondolewa madarakani kwa rais wa zamani Hosni Mubaraka mwaka 2011.

Maandamano yalishuhudiwa katika miji mikuu Cairo na Alexandria mwishoni mwa juma lililopita, huku waandamanaji wakilalamika kuwa tangu kutokea kwa mapinduzi hayo, hakuna mabadiliko ya kweli waliyokuwa wanayapiginia ikiwemo ajira kwa vijana, bado hayajaonekana.

Serikali ilipiga marufuku kuadhimisha kumbukumbu hizo hali iliyosabbaisha vurugu kati ya Waandamanaji na Polisi.

Takriban watu 500 wanashikiliwa kutokana na vurugu hizo, ambazo zimesababisha maafa makubwa tangu kuanza kwa mwaka 2015. Hata hivyo serikali ilipiga marufuku maadhimisho hayo yanayodaiwa kuwa ni ya kumbukumbu ya maandamano ya mwaka 2011.

Maandamano hayo ya mwaka 2011 nchini Misri yalikuwa yakiratibiwa na makundi ya Waislam wenye msimamo mkali ambapo vikosi vya usalama vilishindwa kuwadhibiti waandamanaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.