Pata taarifa kuu
NIGERIA-INEC-BOKO HARAM-Usalama

INEC yapinga kuahirisha uchaguzi Nigeria

Tume ya Uchaguzi nchini Nigeria INEC imesema haitahirisha uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika tarehe 14 mwezi ujao.

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan (kulia), akimpokea kwa mazungumzo Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry (kushoto).
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan (kulia), akimpokea kwa mazungumzo Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry (kushoto). Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa tume hiyo Profesa Attahiru Jega amesema licha ya kupata ombi kutoka kwa washauri wa maswala ya usalama wa rais Goodluck Jonathan kuahirisha uchagauzi huo kwa hofu ya usalama, zoezi hilo litakwenda kama ilivyopangwa.

Upinzani pia umesema hakuna haja ya kuahirsihwa kwa uchaguzi huo kwa kulihofia kundi la Boko Haram linaloendeleza mashambulizi Kaskazini mwa nchi hiyo.

Wapiga kura wanaokadiriwa kuwa milioni 68 watapiga kura kumchagua kati ya rais wa sasa Goodluck Jonathan wa chama tawala cha PDP na Muhamadu Buhari wa chama cha APC.

Jumapili Januari 25 mji wa Monguno, kusini mashariki mwa Nigeria, ulishudiwa mapigano makali kati ya jeshi na wapiganaji wa kundi la Boko Haram.

Jeshi liliingilia kati ili kukabiliana na kuzima mashambulizi ya Boko Haram katika mji wa Maiduguri, ambako kundi hilo lilikua likiendesha mashambulizi kwa lengo la kuyadhibiti maeneo yote ya mji huo.

Hata hivyo wapiganaji wa Boko Haram waliuvamia na kuuteka mji mwengine wa Monguno katika jimbo la Borno.

Haya yalitokea, Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerrry akiwa ziarani nchini humo.

Mwishoni mwa juma lililopita pia iliripotiwa kuwa, wapiganaji hao walijaribu kuiteka miji ya Maiduguri na Konduga kabla ya kutimuliwa na jeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.