Pata taarifa kuu
MALI-MINUSMA-USALAMA

Maandamano dhidi ya Minusma yagubikwa na vurugu

Watu watatu wameuawa katika makabiliano yaliotokea jana mjini Gao kaskazini mwa nchi ya Mali wakati wa maandamano ya kupinga uwepo wa vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini humo Minusma.

Kulingana na msemaji wao, askari wa Umoja wa Mataifa walifyatua risasi hewani kwa lengo la kuwatawanya waandamanaji.
Kulingana na msemaji wao, askari wa Umoja wa Mataifa walifyatua risasi hewani kwa lengo la kuwatawanya waandamanaji. AFP
Matangazo ya kibiashara

Takriban waandamanaji elfu moja walijaribu kupenya na kutaka kujiingiza kwa nguvu katika ngome ya vikosi hivyo na kurusha mawe kabla ya askari hao wa kulinda amani kujibu kwa kupiga mabomu ya machozi ili kuwatawanya.
Katika maandamano hayo watu kadhaa wamejeruhiwa vikali.

Kwa mujibu wa mashahidi, mamia kwa maelfu ya waandamanaji walijaribu kuiingia katika ngome ya vikosi vya Umoja wa Mataifa, lakini walitawanywa na vikosi hivyo.

Msemaji wa Minusma, OlivierSalgado, amesema waandamanaji hawakufyatuliwa risasi za moto, bali wanajeshi wa Umoja wa Mataifa walilazimika kufyatua risasi za plastiki hewani ili kuwatawanya, baada ya kuivamia ngome yao.

Hata hivyo, duzu za hospitali zimethibitisha kwamba watu waliouawa, waliuawa kwa kupigwa risasi za moto. Shughuli zilizorota Jumanne wiki hii katika mji wa Gao kufuatia vurugu hizo. Maduka yalifungwa, visomo katika shule mbalimbali vilisitishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.