Pata taarifa kuu
LIBYA-IS-Ugaidi-Mauaji-Usalama

Shambulio dhidi ya hoteli Corinthia

Watu waliojihami kwa silaha wamewaua watu tisa baada ya kuvamia hoteli moja ya kifahari jijini Tripoli nchini Libya na kuanza kuwafwatulia risasi raia waliokua ndani ya hoteli hio.

Gari ya vikosi vya usalama karibu na hoteli Corinthia katika mji wa Tripoli, Januari 27 mwaka 2015.
Gari ya vikosi vya usalama karibu na hoteli Corinthia katika mji wa Tripoli, Januari 27 mwaka 2015. REUTERS/Ismail Zitouny
Matangazo ya kibiashara

Wataalam wa masuala ya usalama wanasema kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu limeanza kusambaza ushawishi wake katika nchi mbalimbali duniani.

Hoteli hiyo ya Corinthia ni mali ya zamani ya familia ya Gaddafi, ambayo imejengwa katikati ya eneo la kibiashara mjini Tripoli, moja ya maeneo machache, ambayo yamekua yakitembelewa na wanadiplomasia, wanasiasa na watu kutoka nchi za kigeni.

Hata hivyo usalama wa hoteli hio uliingiliwa na dosari mwezi Oktoba mwaka 2013, wakati Waziri mkuu wakati huo, Ali Zeidan, alipotekwa nyara akiwa chumbani mwa hoteli hiyo.

Jana Jumanne, wakati wa shambulio, hoteli hio inayojulikana kwa jina la nyota 5, ilikuwa tupu. Wengi mwa wajumbe wa kigeni waliokua wakiishi katika hoteli hio waliondoka katika mji wa Tripoli katika majira ya joto mwaka uliyopita kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama.

Ripoti zinasema baada ya shambulio hilo, waliowaua watu hao wakiwa raia wa kigeni walijilipua nje ya hoteli hiyo ya Corinthia.

Miongoni mwa waliouawa katika shmabulio hilo ni pamoja na mtalaam wa msewal ya usalama kutoka Marekani pamoja na raia mmoja wa ufaransa.

Kundi la Islamic State katika ukurasa wake wa Twitter umedai kuwa washirika wao ndio waliotekeza mauji hayo.

Raia wa wawili kutoka Tunisia na Sudanm, ambao ni wanamgambo wa kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu ndio walihusika na shambulio hilo.

Marekani na Ufaransa zimethibitisha taarifa hio ya kuuawa kwa raia wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.