Pata taarifa kuu
SOMALIA-AL SHABAB-Usalama

Zakariya Ismail Hersi ajitenga na Al Shabab

Kiongozi wa juu wa kundi la Al Shabab kutoka nchini Somalia Zakariya Ismail Hersi, ametangaza kuwa ameachana na kundi hilo.

Wapiganaji wa kundi la Al Shabab, nchini Somalia.
Wapiganaji wa kundi la Al Shabab, nchini Somalia. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Hersi ambaye alikuwa anatafutwa na wanajeshi wa Umoja wa Afrika na serikali ya Marekani na kujisalimisha mwezi Desemba mwaka jana alikuwa kiongozi wa kitengo cha Inteljensia katika kundi hilo.

Hersi amezungumza kwa mara ya kwanza na kutoa wito kwa wafuasi wengine wa Al Shabab kujisalimisha na kuchagua amani.

Wachambuzi wa maswala ya usalama wanasema, kiongozi huyo wa Al Shabab alijisalimisha kwa kuhofia usalama wake baada ya kuuliwa kwa kiongozi wa juu wa kundi hilo Ahmed Godane, baada ya kushambuliwa na ndege za kivita za Marekani mwaka uliopita.

Hata hivyo kundi la Al Shabab, limebaini kwamba Zakariya Ismail Hersi, alitimuliwa katika kundi hilo tangu kitambu kutokana na ushiriki wake na Idara ya ujasusi ya Somalia pamoja na vibaraka wake.

Serikali ya Somalia imesema itaomba Umoja wa Afrika na Marekani kutomfuatilia kiongozi huyo wa juu wa zamani wa kundi la Al Shabab.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.