Pata taarifa kuu
CAR-ANTI BALAKA-SELEKA-Usalama

Makubaliano yaliyoafikiwa Nairobi yakataliwa Bangui

Makubaliano yaliyotiliwa saini katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi kati ya wafuasi wa marais wa zamani wa jamhuri ya Afrika ya Kati, Michel Djotodia na François Bozizé yamekosolewa na serikali ya Bangui.

Marais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Michel Djotodia (kushoto) na François Bozizé (kulia), Januari 11 mwaka 2013.
Marais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Michel Djotodia (kushoto) na François Bozizé (kulia), Januari 11 mwaka 2013. AFP PHOTO / STEVE JORDAN
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya mpito, ambayo haikushiriki katika mazungumzo kati ya makundi hayo hasimu,imefutilia mbali makubaliano hayo.

Wanadiplomasia wameonyesha picha ya madai yaliyotolewa na wafuasi wa marais hao wawili wa zamani. Kwa upande wa naibu wa mpatanishi Soumeilou Boubeï Maiga, alibaini Jumanne kwamba Nakala ya makubaliano hayo haiwezi kuthibitishwa.

Mjini Nairobi wafuasi wa Michel Djotodia, wakiongozwa na Nourredine Adam, pamoja na wafuasi wa François Bozizé, walitoa madai ambayo yanayoeleweka na ambayo pia yamewashangaza wengi. Makundi hayo hasimu yametangaza kusitisha mapigano, lakini yameomba kusamehewa kwa kwa makosa yanayotuhumiwa, kufanyike mabadiliko ya serikli pamoja na kuweko na serikali mpya ya mpito.

Wafuasi wa makundi hayo hasimu wanataka majeshi yote ya kigeni nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yawekwe chini ya mamlaka ya Umoja wa mataifa, hapa wakilenga kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa (Sangaris). Wafuasi hao wanadai pia kwamba marais wa zamani waruhusiwe kugombea katika uchaguzi ujao, kimesema chanzo ambacho kilipewa nafasi ya kusoma nakala hiyo ya makubaliano.

Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati imesema kwmba haiungi mkono nakala hio, kwani haikushirikishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.