Pata taarifa kuu
NIGERIA-BAGA-MAPIGANO-USALAMA

Baga yarejea mikononi mwa serikali

Jeshi la Nigeria limetangaza kwamba limeurejesha kwenye himaya ya serikali mji wa Baga, kaskazini mashariki mwa nchi.

Zoezi la pamoja kati ya majeshi ya Nigeria na Marekani katika mji wa Lagos Oktoba 18 mwaka 2013.
Zoezi la pamoja kati ya majeshi ya Nigeria na Marekani katika mji wa Lagos Oktoba 18 mwaka 2013. AFP PHOTO/ PIUS UTOMI EKPEI
Matangazo ya kibiashara

Mapema mwezi Januari, mji wa Baga, ulioko katika mwambao wa Ziwa Chad ulianguka mikono mwa kundi la Boko Haram, lililoendesha shambulio ambalo linaaminika kuwa ni la kwanza kuwahi kutokea kwa kipindi cha miaka sita iliyopita, ambalo lililogharimu maisha ya watu wengi.

Baada ya mapigano makali na wapiganaji wa Boko Haram, wanajeshi wa Nigeria waliurejesha mji wa Baga kwenye himaya ya serikali Jumamosi alasiri, jeshi limetangaza kwenye akaunti yake ya Twitter.

Hasara kubwa imetokea katika mapigano hayo, na operesheni ya kuyatafuta mabaki ya wanamgambo hao wa Boko Haram inaendelea, jeshi limeongeza.

Ndani ya kipindi cha mwezi mmoja pekee wa Januari, Boko Haram iliyateka baadhi ya maeneo ya Nigeria, hususan, kambi ya kikosi cha wanajeshi wa kimataifa katika mji wa Baga, kilomita chache kutoka Ziwa Chad, pamoja na mji wa Monguno.

Mji wa Monguno, kusini mashariki mwa Nigeria, ulianguka mikononi mwa kundi la Boko Haram Jumapili Januari 25 mwaka 2015 asubuhi, baada ya mapigano makali kati ya jeshi na wapiganaji wa kundi hilo la Boko Haram.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.