Pata taarifa kuu
MAREKANI-SOMALIA-Diplomasia

Marekani yamteua balozi wake wa kwanza Somalia

Wizara ya Mambo ya nje imetangaza kwamba Rais Obama amemteua balozi wa Marekani nchini Somalia, ikiwa ni tukio la kihistoria kwani Marekani haikua na mwakilishi Mogadidiscio tangu mwaka 1991.

Picha isiyo na tarehe ya ubalozi wa zamani wa Marekani mjini Mogadiscio.
Picha isiyo na tarehe ya ubalozi wa zamani wa Marekani mjini Mogadiscio. DR.
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, Washington, Jean-Louis Pourtet, Rais Obama amemteua Katherine Dhunani, ambaye alikua akisimamia ubalozi mdogo katika mji wa Hyderabad, nchini India, kuwa balozi wa Marekani nchini Somalia.

Mwanamama huyo ataendesha na shughuli zake wakati huu, akiwa katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi. Uamzi huu ni kutokana na hali ya usalama katika mji wa Mogadiscio ambayo haijaimarika.

Kumbukumbu ya kudunguliwa kwa helikopta Black Hawk mwaka 1993 na waasi bao inawatia hofu viongozi wa Marekani. Hata hivyo uteuzi huo utapaswa kuthibitishwa na baraza la Seneti.

Rais wa somalia alipokelewa katika Ikulu ya White House mwezio Januari mwaka 2013, baada ya Washington kuitambua kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1991, serikali ya Somalia.

Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani imekaribisha " maendeleo ya raia wa Somalia kwa kuondokana na miongo kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe".

Waizara ya mambo yanje ya Marekani imebainisha kwa kumesalia mambo mengi ya kufanya ili Somalia iwe ni " taifa la amani, taifa lenye misingi ya kidemokrasia na mafanikio". Mamia ya wanajeshi wa Marekani wanasaidi kwa kutoa mafunzo kwa jeshi la Somalia, na mwezi uliopita, mmoja wa viongozi wa Al-Shabab aliuawa na ndege ya Marekani isiyo na rubani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.