Pata taarifa kuu
DRC-FDLR-USALAMA

Serikali ya DRC yadai kuwakamata waasi zaidi ya 40 wa FDLR

Zaidi ya watu 40 wanaodaiwa na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwa ni wapiganaji wa waasi wa kihutu wa Rwanda walioneshwa Jumapili Machi 1 mwaka 2015 mjini Goma, mashariki mwa nchi hio.

Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) katika operesheni katika kitongoji kimoja cha mji wa Goma, Oktoba 31 mwaka 2013..
Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) katika operesheni katika kitongoji kimoja cha mji wa Goma, Oktoba 31 mwaka 2013.. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Wengi miongoni mwa watu hao wamekiri kuwa ni raia wa Congo. Baadhi walijisalimisha kabla ya kuanza operesheni ya kuwapokonya silaha waasi wa Kihutu wa Rwanda FDLR ambayo ilianza tangu Februari 27 mwaka 2015, na wengine walichukuliwa kama wafungwa wakati wa operesheni hio.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, katika mji wa Goma, Kamanda wa Kamanda Muzembe, watu 23 ni wanadai kuwa ni raia wa Congo na wengine 20 ni raia wa Rwanda.

Hata hivyo viongozi wa jeshi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, raia hao 23 kutoka Congo wanatuhumiwa kuanzisha kundi lenye lengo la kuhatarisha usalama wa taifa.

Viongozi hao wa kijeshi wamebaini pia kwamba raia hao kutoka Rwanda waliokamatwa, wanatuhumiwa kuendesha mashambulizi ndani ya aridhi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakitokea nchi jirani. Msemaji wa serikali akiwa pia waziri wa habari, Lambert Mende, amesema raia hao wa Rwanda watachukuliwa kama wafungwa wa kivita.

Hayo yakijiri jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limebaini kwamba limezindua operesheni ya kuwasaka waasi hao wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR katika mkoa wa Kivu Kaskazini na Kaskazini mwa mkoa wa Katanga.

Operesheni hiyo imezinduliwa mwishoni mwa juma lililopita kwenye milima ya Mugogo, kilomita 10 kaskazini magharibi mwa kijiji cha Rusayo ndani ya hifadhi ya Virunga na kuwafurusha waasi hao na katika maeneo mengine ya wilaya ya Rutshuru na Nyiragongo.

Vyanzo vya ndani wilayani Nyiragongo vimethibitisha kusikika kwa milio ya risasi na silaha nzitonzito kuashiria ukali wa mapambano hayo ambapo mwanajeshi mmoja anaripotiwa kufariki na mwengine kujeruhiwa.

Jeshi la FARDC kwa upande wake limeweka wanajeshi wa kikosi maalumu cha batalion 391 cha mashambulizi ya haraka baina ya eneo la mapambano na makazi ya watu kuepuka uwezekano wowote wa waasi hao kufunga barabara ya Rutshuru kwenda Goma.

Baada ya uzinduzi wa operesheni hiyo dhidi ya waasi wa FDLR Alhamisi tarehe 26 mwezi uliopita wilayani Rutshuru huko jimboni Kivu Kaskazini vyanzo vya kijeshi vimebainisha kuwa tayari makamanda watatu wa waasi hao wamekamatwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.