Pata taarifa kuu
UN-DRC-DPLIOMASIA

Mvutano kati ya UN na DRC unaendelea

Mvutano baina ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) umechukuwa sura nyingine hapo jana katika Baraza la Usalama la umoja huo kuhusu kuondoka au la kwa vikosi vya kulinda amani nchini humo MONUSCO.

Picha inaonyesha helikopta ya mashambulizi ya MONUSCO, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo.
Picha inaonyesha helikopta ya mashambulizi ya MONUSCO, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo. Photo MONUSCO/Force
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Congo Raymond Tshibanda amesema kuwa wakati umefika kwa nchi yake kuwajibika kikamilifu kwa ajili ya usalama wa nchi yake akiliomba baraza hilo kuheshimu dhamira ya serikali ya Kinshasa kwa kuamuru MONUSCO waanze kuondoka kwa awamu.

Aidha, waziri huyo amesema kuwa maendeleo ya kisiasa na kiuchumi yaliyoletwa na serikali yake ni mafanikio makubwa, huku akidai kuwa makabiliano ya vikosi vya serikali dhidi ya waasi wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR mashariki mwa DRC yanaendelea kushika kasi.

Akizungumza kwa niaba ya Umoja wa Mataifa, mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa na mkuu wa vikosi hivyo vya MONUSCO, Martin Kobler, amesisitiza kwamba kwa ujumla hali ya usalama imeimarika na kwamba bado yako maeneo mengi ya kufanyia kazi mashariki mwa nchi hiyo ambako raia wanaishi katika hofu.

Kulingana na vyanzo vya kidiplomasia, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lina mpango wa kupunguza vikosi hivyo kwa kiwango cha askari elfu mbili kati ya elfu ishirini walioko Congo wakati serikali ya Kinshasa ikisema kiwango cha kwanza cha wataokaoondoka kitakua cha askari elfu sita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.