Pata taarifa kuu
TUNISIA-USALAMA

Mkanganyiko waibuka kuhusu uzinduzi wa jumba la maonyesho nchini Tunisia

Shughuli za uzinduzi wa eneo la maonyesho ya kitalii nchini Tunisia zimeahirishwa hadi tarehe ambayo haikutangazwa bado, lakini sherehe za kuwakumbuka wahanga 21 waliopoteza maisha mwishoni mwa juma lililopita katika shambulio liliendeshwa na kundi la Islamic State.

Polisi akipiga doria karibu na jumba la maonyesho la Bardo jijini Tunis.
Polisi akipiga doria karibu na jumba la maonyesho la Bardo jijini Tunis. REUTERS/Anis Mili
Matangazo ya kibiashara

kumekuwa na mkanganyiko kuhusu sababu za kuahirishwa kwa tarehe ya uzinduzi wa maeneo hayo yaliotangazwa kuzinduliwa jumanne hii na viongozi wa taifa hilo. Uongozi wa eneo la maonyesho hayo umesema sababu za kiusalama, huku serikali ikikanusha na kusema kwamba ni kuotkana na ukarabati ambao bado haujakamilika.

Waziri wa maswala ya utamaduni nchii Tunisia alieleza sababu za mpangilio wa sherehe hizo ndio zimesababisha kuahirishwa. Sherehe rasmi zilipangwa kufanyika hii leo mchana ambapo bendi ya muziki ingetumbwiza ili kutowa heshima kwa watu 20 raia wa kigeni pamoja na polisi 1 wa Tunsia waliofariki katika shambulio hilo.

Mofdi Mssedi, anaehusika na maswala ya mawasiliano katika ofisi ya waziri mkuu wa Tunisia Habib Essib amesema jengo hilo la makumbusho litazinduliwa hivi karibuni baada ya kukamilika kwa shughuli za ukarabati na kwamba usalama umeimarika vya kutosha.

Viongozi wa jengo hilo walikuwa wameariku kwamba hapakuwa na shughuli kubwa za ukarabati wa jengo hilo baada ya kutokea kwa shambulio lililotekelezwa na watu 2 waliokuwa na silaha aina ya kalachinikov na ambao waliuawa baada ya kutekeleza mauaji ya watu 21.

shambulio hilo lilizua ukosoaji mkubwa kuhusu swala la usalama katika eneo la jengo hilo pamoja na ofisi za bunge zilizopo katika eneo hilo, wakati huu mshukiwa mwingine wa 3 akiendelea kusakwa kwa udi na uvumba.

Waziri mkuu wa Tunisia Habib Essib hapo jana aliwafuta kazi viongozi kaza wa idara ya usalama akiwemo kiongozi wa polisi jijini Tunis pamoja na Bordo, huku polisi mmoja wa usalama katika jengo la makumbusho akitiwa mbaroni kwa sababu ambazo hazikuwekwa bayana.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.