Pata taarifa kuu
AFRIKA-MISITU-TEMBO-MAZINGIRA

Tembo wa Afrika huenda wakatoweka hadi miaka 20 ijayo

Tembo walioko bara la Afika huenda wakatoweka kabisa katika kipindi cha miongo michache ijayo, wataalamu wameonya wakati huu mkutano wa kimataifa kuhusu wanyama pori na viumbe adimu duniani ukifanyika nchini Botswana.

Tembo wa Afrika katika muda mfupi wanaweza kutoweka porini, tembo hawa ni waathirika wa ujangili kwa pembe za ndovu, wameonya wataalam wanaokutana Jumatatu Machi 24 mwaka 2015 Botswana.
Tembo wa Afrika katika muda mfupi wanaweza kutoweka porini, tembo hawa ni waathirika wa ujangili kwa pembe za ndovu, wameonya wataalam wanaokutana Jumatatu Machi 24 mwaka 2015 Botswana. AFP/Roberto SCHMIDT
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu uliopewa jina Tembo wa Afrika, unafanyika katika mji wa kitalii wa Kasane ambapo wajumbe toka zaidi ya nchi 20 kutoka barani Ulaya, Afrika, Asia ikiwemo na China ambayo inatuhumiwa kuhusika na biashara haramu ya pembe za ndovu duniani.

Wataalamu wanasema, wanyama hawa huenda wakatoweka kabisa katika kipindi cha miaka mitano au kumi ijayo iwapo hali inayoshuhudiwa sasa itaendelea kuachiwa bila hatua kuchukuliwa.

Carlos Drews ambaye ni mkurugenzi wa shirika la kimataifa la uhifadhi wa wanayama pori anayehusika na programu maalumu kuhusu viumbe hai, amesema wameridhishwa na hatua zinazochukuliwa na baadhi ya mataifa licha ya kuwa bado kuna hatari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.