Pata taarifa kuu
LIBYA-WAHAMIAJI-ULAYA-USALAMA

Libya, nchi ya mapokezi kwa wahamiaji haramu

Machafuko yanaendelea kushuhudiwa nchini Libya, nchi ambayo imeendelea kukumbwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Wahamiaji wakisubiri kuvuka Mediterranean,Tripoli Machi 13 mwaka 2015.
Wahamiaji wakisubiri kuvuka Mediterranean,Tripoli Machi 13 mwaka 2015. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Libya kwa sasa ina taasisi mbili za Bunge pamoja na serikali mbili, huku nchini humo kukiendelea kushuhudiwa utitiri wa wahamiaji wanaojielekeza Ulaya.

Kwa kipindi kirefu Libya imekua ikiwapokea wahamiaji kutoka kusini mwa jangwa la Sahara, lakini kwa sasa nchi hiyo ni sehemu ya kuotea mbali.

Mwaka 2010, rais wa zamani wa Libya hayati Muammar Gaddafi alikua akionya Ulaya kufuatia wimbi la wahamiaji haramu wa kiafrika ambao walikua wakikimbilia kwa wingi barani Ulaya, huku akidai dola bilioni tano ili kuwazuia wahamiaji wanatoka Afrika kusini mwa Sahara kuendelea kukimbilia Ulaya.

Wakati huo alionekana kuchukua umazi wa mwisho wa kuwazuia wahamiaji kutoka Afrika kuendela kukimbilia Ulaya kwa kuogopa wimbi la wahamiaji. Lakini kiongozi huyo hakuwahi kusema kuwa nchi yake imekua ni sehemu ya mapokezi ya wahamiaji kuelekelea Ulaya.

Kabla ya mabadiliko ya tawala na vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi mbalimbali za kiarabu, Libya ilikua ikipokea zaidi ya milioni mbili za wahamiaji haramu, wakitokea hasa Tunisia, Misri na nchi za kusini mwa Sahara. Wakati huu, wahamiaji wengi ni kutoka hasa Afrika Mashariki: Ethiopia, Eritrea, Sudan na Somalia. Barabara zinazopita Azores, Morocco na Algeria kwa sasa zinalindwa kwa umakini. Kwa hiyo waahamiaji hao wamekua wakiamua kupitia Libya. Kati ya wahamiaji 300 na 700 waondoka kila siku Libya wakielekea Ulaya.

Zaidi ya wahamiaji 11,000 waliokuolewa kwa kipindi cha wiki moja, huku zaidi ya wahamiaji 700 wakifariki kufuatia kuzama kwa boti waliyokuwemo usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili mwishoni mwa juma hili lililopita katika pwani ya Libya.
Kufuatia hali hiyo, mawaziri wa mambo ya nje wa Ulaya walikutana Jumatatu Aprili 20 mjini Luxemburg ili kujadili uwezekano wa kudhibiti hali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.