Pata taarifa kuu

Edouard Nduwimana: “polisi yatumia risasi za moto”

Waziri wa mambo ya ndani wa Burundi Edouard Nduwimana amekiri kuwa polisi imekua ikitumia risasi za moto kwa kuwalenga waandamanaji wakati wa maandamano ya kupinga muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza.

Waandamanaji wanasema kwamba kulingana na Katiba ya Burundi, Rais Pierre Nkurunziza hawezi kuwania muhula wa tatu.
Waandamanaji wanasema kwamba kulingana na Katiba ya Burundi, Rais Pierre Nkurunziza hawezi kuwania muhula wa tatu. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati naibu Waziri wa maswala ya Haki za Binadamu na Demokrasia wa Marekani, Tom Malinowski, alikutana jana na viongozi mjini Bujumbura nchini Burundi kuzungumzia hali ya kisiasa nchini humo, baada ya rais Piere Nkurunziza kutangaza kuwania urais kwa muhula wa tatu.

Kabla ya majadiliano hayo na viongozi wa Burundi naibu Waziri huyo amesema kwenye akaunti yake ya Twitter kuwa amekatishwa tamaa "kuona Rais Pierre Nkurunziza amekiuka Azimio lililosainiwa mwishoni mwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2006, na kusisitiza kuwa wahusika wa ghasia zilizojitokeza watawajibika.

Wakati huohuo, Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Burundi Edouard Nduwimana ametoa wito kwa utulivu na kuwaomba raia wao waliokimbilia nchi jirani ya Rwanda kurudi nyumbani, huku akikariri kwamba polisi wakati mwingine wametumia risasi za moto.

Sanjari na hayo, maseneta kumi na wanne, wote kutoka chama tawala cha CNDD-FDD wamehoji hapo Jumatano wiki hii mbele ya mahakama ya kikatiba uhalali wa pingamizi ya upinzani dhidi muhula wa tatu wa rais Nkurunziza, hatua ambayo inatupiliwa mbali na Upinzani kwa vile Jumuiya ya kimataifa inafahamu kuwa hatua ya Nkurunziza ni kinyume na katiba.

Pamoja na hayo, wimbi la wakimbizi kutoka Burundi linaendelea kushuhudiwa katika Wilaya ya Fizi nchini DRC, wengi wao wakitokea maeneo ya vijijini, katika miko mbalimbali ya magharibi mwa Burundi.

Pamoja na kutoa wito kwa utulivu na kuwaomba wananchi warudi makwao, serikali ya Burundi imeyafunga makazi ya wananfunzi wa vyuo vikuu vya mjini Bujumbura kufwatia matukio ya hivi karibuni, hatua itakayoanza kutekelezwa leo Jumatatu asubuhi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.