Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAANDAMANO-USALAMA-SIASA

Burundi: jeshi lawaonya wanasiasa

Waziri wa Burundi mwenye dhamana ya ulinzi, Pontien Gaciyubwenge amewaonya wanasiasa na taasisi za nchi kuheshimu Mkataba wa amani wa Arusha na Katiba ya nchi hiyo.

Mwanajeshi akipita katikati ya halaiki ya waandamanaji wakati wa makabiliano kati ya vijana waandamanaji na polisi, Bujumbura, Jumatatu Aprili 27 mwaka 2015. Wanajeshi wanasema wamekuja  "kuliwandia usalama raia".
Mwanajeshi akipita katikati ya halaiki ya waandamanaji wakati wa makabiliano kati ya vijana waandamanaji na polisi, Bujumbura, Jumatatu Aprili 27 mwaka 2015. Wanajeshi wanasema wamekuja "kuliwandia usalama raia". REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Katika tangazo alililotoa Jumamosi mwishoni mwa juma hili, Waziri Gaciyubwenge amepongeza wanajeshi kwa msimamo walioonyesha wakati wamaandamano ya raia wakipinga uteuzi wa rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu wa urais.

Tangazo hilo la waziri Gaciyubwenge linakuja siku moja baada ya mashirika ya kiraia na upinzani kuwataka raia kusitisha maandamano kwa muda wa siku mbili tangu Jumamosi Mei 2 ili kumpa nafasi rais Pierre Nkurunziza aweze kufikiria kujiondoa katika kinyanganyiro cha kuwania urais.

Waziri Gaciyubwenge ameelezea maskitiko yake kuhusu mauaji ya mwanajeshi aliyeuawa Alhamisi wiki hii na afisa wa Idara ya Ujasusi wilayani Musaga, pamoja na raia walioyouawa na wengine kujeruhiwa tangu maandamano yalipoanza Jumapili mwishoni mwa juma lililopita.

Waziri Gaciyubwenge amewataka wanajeshi kuendelea kuwalindia usalama raia, huku akikumbusha kwamba, jeshi halitokubali mtu yeyote kuvunja Mkataba wa amani wa Arusha pamoja na Katiba ya nchi hiyo kwa maslahi yake. Amewaonya pia watu ambao wamekua wakitumia kauli mbovu za kutenganisha raia, kuwatia uoga na vitisho pamoja na uchochezi wa ubaguzi wa kikabila.

Wakati huo huo, watu watatu ikiwa ni pamoja na maafisa wawili wa polisi wameuawa kwa gruneti usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi mwishoni mwa juma hili na watu wasiojulikana wilayani Kamenge, Kaskazini mwa jiji la Bujumbura, siku moja baada ya mwanajeshi kuuawa na afisa wa Idara ya Ujasusi wilayani Musaga kusini mwa Bujumbura. Hata hivyo mlipuko mwengine wa gruneti uliwajeruhi askari polisi wengine kando na soko kuu la zamani la Bujumbura usiku wa kuamkia Jumamosi Mei 2 mwaka 2015.

Wadadisi wanaona kuwa huenda shambulizi hilo ni kazi ya waandamanaji lakini yaweza kuwa pia mbinu ya maofisa kuelezea madai ya kuwa waandamaji wanatumia silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.