Pata taarifa kuu
BURUNDI-KORTI-USALAMA-SIASA

Burundi: naibu mkuu wa Korti ya Katiba aikimbia nchi

Naibu mkuu wa Korti ya Katiba nchini Burundi, Sylvère Nimpagaritse, ameikimbia nchi yake kutokana na kile alichokiita nguvu za kupita kiasi zinazotumiwa na utawala pamoja na vitisho vya kuuawa vilivyokua vikimkabili.

Waandamanaji wanasema kwamba kulingana na Katiba ya Burundi, Rais Pierre Nkurunziza hawezi kuwania muhula wa tatu.
Waandamanaji wanasema kwamba kulingana na Katiba ya Burundi, Rais Pierre Nkurunziza hawezi kuwania muhula wa tatu. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Kukimbia kwa kiongozi huyo ni pigo kubwa kwa Pierre Nkurunziza, baada ya kuteuliwa na chama chake cha Cndd-Fdd kuwania muhula wa tatu katika uchaguzi wa urais.

Wiki iliyopita baadhi ya Maseneta kutoka chama hicho tawala waliwasilisha waraka mbele ya Korti ya Katiba wakiomba kutoa uamzi kuwania muhula wa tatu au la kwa rais Pierre Nkurunziza. Tukio hili limewashangaza wengi nchini Burundi.

Sylvère Nimpagaritse, ameikimbia nchi yake Jumatatu Mei 4 mwaka 2015. Kukimbia kwa naibu mkuu wa Korti ya Katiba kumeibua hisia tofauti katika chama tawala cha Cndd-Fdd, hasa kwa wale wanaomuunga mkono Rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.

Baadhi wanasema Sylvère Nimpagaritse, ni mtu mwenye uoga, lakini mwenye dhamira na msimamizi mbele ya jambo fulani linapojitokeza.

Sylvère Nimpagaritse, ameeleza kwamba Korti ya Katiba ilianza kushughulikia suala kuhusu muhula wa tatu wa rais Alhamisi juma lililopita. Wakati huo majaji wanne kati ya saba wa Korti ya Katiba walipinga muhula watatu wa Rais Pierre Nkurunziza, wakibaini kwamba ni kinyume na Katiba ya Burundi pamoja na Mkataba wa amani na maridhiano wa Arusha.

Sylvère Nimpagaritse, amesema tangu wakati huo, majaji waliopinga muhula mwengine wa Pierre Nkurunziza walianza kupata vitisho vya kuuawa. Majaji watatu kati ya wanne waliokua na msimamo wa kupinga muhula wa tatu wa rais Nkurunziza waliamua kukimbilia nje ya nchi kwa kuhofia usalama wao, amesema Sylvère Nimpagaritse, huku akibaini kwamba tangu wakati huo alibaki mwenyewe. " Lakini kwa sasa nimefaulu kuikimbia nchi ", amesema Sylvère Nimpagaritse

Hayo yakijiri watu watatu wameuawa Jumatatu wiki hii katika maandamano yaliyofanyika mjini Bujumbura, huku wengine zaidi ya arobani wakijeruhiwa. Mpaka sasa watu kumi nambili ndio wameuawa tangua maandamano ya kupoinga Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu kuanza wiki moja iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.