Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAANDAMANO-USALAMA-SIASA

Maandamano yashuhudiwa Bujumbura

Marekani imepinga Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kuwania muhula watatu. kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, Rais Pierre Nkurunziza hana haki ya kuwania muhula wa tatu, na ni kinyume na Katiba ya Burundi, amesema Kerry.

Polisi na waandamanaji uso kwa uso, wlayani Musaga, kusini mwa Bujumbura, Mei 4 mwaka 2015.
Polisi na waandamanaji uso kwa uso, wlayani Musaga, kusini mwa Bujumbura, Mei 4 mwaka 2015. RFI/SR
Matangazo ya kibiashara

Kauli hiyo ya Kerry inakuja baada ya siku mbili ya kusitishwa kwa maandamano mjini Bujumbura tangu Jumamosi mwishoni mwa juma hili lililopita. Jumatatu Mei 4, raia kutoka wilaya mbalimbali za mji wa Bujumbura wameingia kwa mara nyingine mitaani wakipinga uteuzi wa Rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.

Makabiliano makali yameshuhudiwa Jumatatu mchana kati ya polisi na waandamanaji. Polisi imewafyatulia risasi za moto waandamanaji, na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine zaidi ya 45 kujeruhiwa, kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu.

Hata hivyo waandamanaji wenye hasira wamesadikiwa kuchoma nyumba ya askari polisi mmoja wilayani Musaga, kusini mwa jiji la Bujumbura.

Jipya katika maandamano ya Jumatatu wiki hii, raia wa baadhi ya wilaya za mikoa ya Bujumbura, Bururi na Mwaro, katikati mwa Burundi wameungana na wenzao wa manispa ya jiji la Bujumbura kwa kuandamana wakipinga muhula wa tatu wa Pierre Nkurunziza.

Wakati huo huo baadhi ya waandamanaji wamepenya na kuingia katikati mwa mji wa Bujumbura, lakini polisi imefaulu kuwatawanya. Waandamanaji kadhaa wamekamatwa.

Inaarifiwa pia kuwa askari polisi wawili wameuawa katika maandamanao hayo, baada ya kufyatuliwa risasi na watu wasiojulikana.

Hivi karibuni baadhi ya maseneta kutoka chama cha Cndd-Fdd wanaomuunga mkono Rais Pierre Nkurunziza waliwasilisha waraka mbele ya Korti ya kikatiba wakiiomba Korti hiyo ichukuwe uamzi iwapo Rais Nkurunziza ana haki ya kuwania muhula mwengine au la. Korti hiyo inasubiriwa kutoa uamzi wake leo Jumatatu jioni au Jumanne wiki hii. Hakuna mshangao wowote iwapo Korti hiyo itaamua Rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu, kwani inasadikiwa kuwa majaji wote sabaa wa Korti hiyo ni vibaraka wa rais huyo.

Hatua hiyo ikipita, Pierre Nkurunziza ataamua haraka iwezekanavyo iwapo atawania au la muhula wa tatu katika uchaguzi wa urais, licha ya kuwa waandamanaji wameapa kuendelea na maandamano iwapo Rais Nkurunziza ataendelea na msimamo wake wa kuwania muhula wa tatau wa urais

Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake kufuatia hali ya usalama inayoendelea kudorora nchini Burundi. Umoja wa Mataifa umezitaka pande husika kuketi kwenye meza ya mazungumzo haraka iwezekanavyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.