Pata taarifa kuu
UJERUMANI-RWANDA-MAUAJI-SHERIA-HAKI

kesi ya Onesphore Rwabukombe yafunguliwa upya

Mahakama nchini Ujerumani imeamuru kufunguliwa upya kwa kesi dhidi ya Onesphore Rwabukombe, aliyekuwa Meya wa Muvumba nchini Rwanda wakati wa mauaji ya kimbari mwaka 1994.

Onesphore Rwabukombe, Meya wa zamani wa Muvumba, anakabiliwa na kifungo cha maisha jela kwa kuhusika katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda, mwaka 1994.
Onesphore Rwabukombe, Meya wa zamani wa Muvumba, anakabiliwa na kifungo cha maisha jela kwa kuhusika katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda, mwaka 1994. AFP PHOTO/DPA/FRANK RUMPENHORST GERMANY OUT
Matangazo ya kibiashara

Mwaka uliopita, Mahakama hiyo ilimhukumu Rwabukombe miaka 14 jela baada ya kupatikana na kosa la kushiriki na kuchochea mauaji hayo.

Jörg-Peter Becker, rais wa Mahakama hiyo amesema baada ya kusikilizwa tena kwa kesi hiyo Rwabukombe huenda akapewa kifungo cha maisha jela.

Zaidi ya watu 800,000 kutoka Jamii ya Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa mwaka 1994 nchini Rwanda baada ya kifo cha rais wa nchi hiyo Juvénal Havyarimana.

Wanamgambo wa chama tawala wakati huo cha MRMD, Interahamwe pamoja na washirika wao kutoka vyama vya Kihutu vyenye msimamo mkali Ikiwa ni pamoja na Palmehutu Pawa walituhumiwa kuhusika katika mauaji hao.

Wengi mwa watuhumiwa hao walikimbilia nchi jirani ya Congo na wengine katika mataifa mbalimbali ya Afrka, Ulaya, na kungineko.

Baadhi yao wamekua wakikamatwa na kuhukumiwa na vyombo vya sheria, huku wengine wakizuiliwa katika jela mbalimbali nchini Rwanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.