Pata taarifa kuu
DRC-UDPS-SIASA

UDPS yakubali kushiriki katika mazungumzo ya kisiasa

Chama cha upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo UDPS kimekubali kushiriki katika mazungumzo ya kisiasa yaliyopendekezwa na rais Joseph Kabila kuelekea uhaguzi mkuu mwaka ujao.

Etienne Tshisekedi kiongozi wa kihistoria wa chama kikuu cha upinzani cha UDPS nchini Congo.
Etienne Tshisekedi kiongozi wa kihistoria wa chama kikuu cha upinzani cha UDPS nchini Congo. AFP PHOTO/GWENN DUBOURTHOUMIEU
Matangazo ya kibiashara

Chama hicho cha mwanasiasa mkongwe Etienne Tshisekedi ambaye yupo Ubelgiji anakopata matibu toka mwezi Agosti mwkaa jana, kimesema kuwa njia pekee ya kupata suluhu ya kisiasa nchini humo ni kupitia mazungumzo.

Hata hivyo vyama vingine vya kisiasa vimesema kuwa havitashirki katika mazungumzo hayo ya kisiasa na rais Joseph Kabila wakati huu joto la kisiasa likiendelea kupanda nchini humo.

Upinzani unamshutumu rais Kabila kuwa na mpango wa kubadilisha kabitiba na kuendelea kuongoza nch hiyo.

hayo yakijiri mtu mmoja ameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mashambulizi yanayosadikiwa kutekelezwa na kundi la wapiganaji wanaomiliki silaha katika mji wa Muhoza wilayani Kalehe mkoani Kivu ya Kusini mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, huku watu wengine wanne hawajulikani waliko.

Mashambulizi hayo yanafanyika siku chache baada ya kuuawa kwa afisa mkuu wa majeshi ya serikali wilayani humo, hali ambayo imesababisha wasiwasi mkubwa katika eneo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.