Pata taarifa kuu
MADAGASCAR-BUNGE-UTAWALA-Siasa

Madagascar : wabunge wapiga kura ya kujiuzulu kwa rais

Mvutano wa kisiasa umejitokeza nchini Madagascar. Wabunge 121 kwa jumla ya wabunge 125 walioshiriki kikao cha Bunge Jumanne wiki hii, wamepiga kura ya kujiuzulu kwa rais wa nchi hiyo Hery Rajaonarimampianina, mwaka mmoja na nusu baada ya kuchaguliwa kwake kuliongoza taifa hilo.

Rais wa Madagascar, Hery Rajaonarimampianina, Januari mwaka 2014.
Rais wa Madagascar, Hery Rajaonarimampianina, Januari mwaka 2014. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Wabunge hao wanamtuhumu rais Hery Rajaonarimampianina kwamba amekiuka katiba ya nchi. Rais huyo anaonekana kupoteza imani kwa wabunge hao.

“ Hajui majukumu yake, hawezi kuliongoza taifa la Madagascar ”, wamesema baadhi ya wabunge. Tuhuma hizo dhidi ya rais Hery Rajaonarimampianina zimeibuka katika kikao cha Bunge cha Jumanne jioni wiki hii, ambapo kikao hicho kiligubikwa na mvutano. Baada ya kikao, baadhi ya wabunge walitaka kuzipiga, na hali hiyo ikapelekea wanajeshi wanaolinda jengo la Bunge kuingilia kati ili kuzuia rabsha isitokei.

Wakiwa na hasira, wabunge hao wamemkosoa rais kwamba hana uamzi katika majukumu yake. Ilimpasa zaidi ya miezi miwili ili kupata waziri mkuu, kabla ya kumfuta kazi baada ya miezi minane. Mahakama Kuu ambayo ingeliundwa katika kipindi cha mwaka mmoja baada ya uchaguzi wa rais haijaundwa. Herry Rajaonarimampianina pia anatuhumiwa kujaribu kushawishi kazi ya wabunge.

Kazi kubwa kwa Mahakama Kuu ya Katiba

Lakini hasira za wabunge zililipuka baada vikao vya kuboresha Maridhiano, vilivyohitimishwa wiki tatu zilizopita. Hakuna mbunge aliyealikwa miongoni mwa washiriki 2,000 waliohudhuria vikao hivyo. Na kuvunjwa kwa Bunge ilikuwa miongoni mwa mapendekezo ya mwisho ya vikao hivyo. Kura iliyopigwa Jumanne wiki hii ina kinga fulani kwa wabunge.

Mahakama ya Katiba (HCC) na majaji wake tisa ndio wana majukumu ya kuthibitishwa au la kwa kujiuzulu katika siku zijazo kwa rais huyo.

Herry Rajaonarimampianina bado ni rais mpaka pale uamzi wa Mahakama ya Katiba wa kujiuzulu kwa rais huyo utatolewa. Inasemekana kuwa majaji wa Mahakama ya Katiba ni washirika wa karibu wa utawala.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.