Pata taarifa kuu
MADAGASCAR-BUNGE-UTAWALA-Siasa

Rais wa Madagascar : “ ni kwa Korti kuu ya katiba kuamua ”

Rais wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina ametupulia mbali pendekezo llililopitishwa na wabunge la kumtaka ajiuzulu.

Wabunge wa Madagascar mbele ya majenngo ya Korti kuu ya Katiba wakiwasilisha barua yao inayomtaka rais Hery Rajaonarimampianina kujiuzulu, Mei 27 mwaka 2015.
Wabunge wa Madagascar mbele ya majenngo ya Korti kuu ya Katiba wakiwasilisha barua yao inayomtaka rais Hery Rajaonarimampianina kujiuzulu, Mei 27 mwaka 2015. AFP PHOTO/RIJASOLO
Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano na waandishi wa habari, Hery Rajaonarimampianina hakubanisha iwapo ataheshimu utaratibu wa kujiuzulu uliyopendekezwa na wabunge dhidi yake. Amesema utaratibu huo utatokana na uamzi wa Korti kuu ya Katiba.

Wabunge wamependelea kwenda haraka. Waraka wa kumtaka rais Hery Rajaonarimampianina kujiuzulu uliwasilishwa na wabunge hao Jumatano mchana wiki hii kwenye ofisi ya makarani wa Korti kuu ya Katiba. Korti kuu ya Katiba itachukua uamzi kwa niaba ya Mahakama kuu ya vyombo vya sheria, ambayo inayo majukumu ya kushughulikia kesi hiyo kulingana na Katiba ya Madagascar, lakini taasisi hiyo haijaundwa nchini humo.

Kutokuwepo kwa Mahakama kuu ya vyombo vya sheria ni moja ya makosa anayotuhumiwa rais Hery Rajaonarimampianina. Rais huyo alikua na muda wa mwaka mmoja wa kuunda taasisi hiyo baada ya kuchaguliwa kwake, lakini sasa miezi sita imemalizika, baada ya muda huo kukamilika.

Korti kuu ya Katiba inatazamiwa kukutana ili kuchukua uamzi wa kuweka muda wa kusubiri barua ya utetezi wa rais Hery Rajaonarimampianina, ambaye anaona kuwa madai ya wabunge hayana msingi wowote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.