Pata taarifa kuu
RFI-CHAD-KUFUKUZWA

Mwandishi wa RFI afukuzwa Chad

Laurent Correau, mwandishi wa RFI aliyetumwa nchini Chad, alifukuzwa nchini humo Jumanne usiku. Mwandishi huyo alikamatwa na maafisa wawili wa Idara ya uhamiaji akiwa ndani ya hoteli ambamo alikua alifikia mjini Ndjamena, na kupelekwa moja kwa moja kwenye uwanja wa ndege, huku akilazimishwa kuingia ndani ya ndege iliyokua ikielekea Paris.

Photo d'un marché dans la capitale tchadienne, Ndjamena
Photo d'un marché dans la capitale tchadienne, Ndjamena EU-AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Laurent Correau alikuwa nchini Chad kuandaa mfululizo wa ripoti juu ya ufunguzi wa kesi ya rais wa zamani wa Chad Hissène Habré uliopangwa kufanyika Julai 20 mjini Dakar.

Ilikua saa nne usiku wakati watu wawili waliodai kuwa maafisa wa Idara ya uhamiaji walipoingia hotelini ambamo Laurent Correau alikua alifikia. Mwandishi huyo wa habari wa RFI alikua akiketi katika mgahawa wa hoteli hiyo na Reed Brody, msemaji wa Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch.

Kwa mujibu wa mashahidi katika eneo la tukio, maafisa hao wawili walimueleza Laurent Correau kufukuzwa kwake kutoka Chad, bila maelezo au hati rasmi.

Mwandishi huyo wa RFI alijaribu kupigia simu viongozi mbalimbali nchini Chad bila mafanikio, kwani maafisa hao hawakumruhusu aendelee kupiga simu. Maafisa hao wa Idara ya Uhamiaji hatimaye walimuonesha beji ambapo Reed Brody alijaribu kuipiga picha. Kitendo hicho cha kupiga picha kiliwakasirikisha maafisa hao. Wakati huo huo Reed Brody na Laurent Correau walipigwa vibao na kumlazimisha mwanahabari wa RFI kunyanyuka na kupelekwa hadi kwenye uwanja wa ndege wa Ndjamena, na baadae kuingizwa ndani ya ndege bila miwani yake, ambayo iliopotea katika purukushani hizo.

Hakuna sababu

Balozi wa Ufaransa, ambaye aliwasili kwenye uwanja wa ndege aliweza kumuona mwanahabari mwenzetu, lakini hakuweza kuzungumza naye. Usiku wa manane, ndege ya Air France iliondoka Ndjamena ikiwa na abiria mbalimbali akiwemo mwandishi wa RFI Laurent Correau.

Uongozi wa RFI unalaani na kupinga kufukuzwa kwa Laurent Correau ambapo mpaka sasa hakuna sababu zilizotolewa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.