Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-BASHAR-ICC-SHERIA

Mahakama: “ serikali ya Afrika Kusini yapaswa kufunguliwa mashtaka ”

Mahakama nchini Afrika Kusini inataka viongozi wa mashtaka kuishtaki serikali kwa kumruhusu rais wa Sudan Kundoka nchini humo na kukiuka amri ya Mahakama.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, Februari 19 mwaka 2015, Bungeni, wakati akilihutubia taifa.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, Februari 19 mwaka 2015, Bungeni, wakati akilihutubia taifa. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Bashir anayetafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya ICC kwa makosa ya ya mauaji katika nchi yake alikuwa nchini Afrika Kusini hivi karibuni kuhudhuria mkutano wa umoja wa Mataifa na kuodoka licha ya Mahakama ya ICC kuitaka serikali ya Afrika Kusini kumkamata.

Jaji wa Mahakama kuu jijini Pretoria Dunstan Mlambo amesema kuwa serikali imekiuka Katiba pamoja na majukumu yake ya kimataifa kwa kutomkamata Bashir.

Hivi karibuni upinzani nchini Afrika Kusini uliomba uchungunzi uendeshwe kubaini ni kwanini serikali haikumkamata rais wa Sudan Omar Al Bashir na kumsafirisha katika Mahakama ya ICC mjini Hague.

Chama cha Democratic Alliance kimesema kinataka kiongozi wa mashtaka kuweka wazi majina ya maafisa wa serikali walioamuru rais Bashir kupewa ulinzi na kufanikiwa kuondoka.

Mahakama ya Afrika Kusini, iliombwa na shirika lisilo la kiserikali la Southern Africa Litigation Center, kumzuia rais wa Sudan ili asiwezi kuondoka nchini humo, angalau mpaka Jumatatu wiki hii.

Shirika hilo liliiomba Mahakama ya Afrka Kusini kumzuia rais Omar al-Bashir na kumsafirisha hadi kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kivita (ICC). Kufuatia ombi hilo, Mahakama ya Pretoria ilikua ilimzuia rais wa Sudan kutothubutu kuondoka nchini Afrika Kusini mpaka vyombo vya sheria vitoe uamzi wake wa mwisho.

Waziri ya mambo ya ndani wa Afrika Kusini alikua alitakiwa kufuatilia kwa karibu maeneo yote hususan mipaka ambapo rais Omar al-Bashir angeliweza kupitia kwa kuondoka nchini Afrika Kusini usiku wa Jumapili Juni 14.

Mwanzoni mwa wiki hii serikali ya Afrika Kusini ilivunja ukimya wake baada ya sakata la Omar al-Bashir. Kwa mujibu wa Phumla Williams, msemaji wa serikali, taarifa hii imeshapitwa na wakati.

“ Tunafutilia mbali taarifa zinazosema kuwa kuna mkutano uliyofanyika, kwa hiyo tutawasilisha ripoti yetu ya uchunguzi, kama ilivyotuomba Mahakama ya Pretoria. Hakuna jaribio lolote, kutoka kwetu kwa kuficha chochote kile. Walituomba tufanye uchunguzi , na ndivyo tunafanya, na tutatekeleza ahadi zetu ”, amesema Phumla Williams.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.